Baada ya klabu ya Simba kuwa na mwenendo usiovutia kwa karibu msimu wa tatu mfululizo, yametolewa maoni mbalimbali na sababu lukuki kuhusiana na nini hasa kiini cha kuvurunda huku. Mojawapo kati ya sababu kubwa ambazo nimezisikia kwa muda mrefu ni kutokuwa fit kimwili kwa wachezaji wa Simba kiasi cha kupelekea kuchoka kadri muda unavyoendelea na kushindwa kuhimili mapambano ua muda mrefu.
Mmojawapo wa watoa hoja hiyo ni Mtemi Ramadhani kiungo nguli wa Simba wa miaka ya nyuma ambaye nimesikia mara nyingi akilirudia sababu hii na pia baadhi ya makocha na wachambuzi mbalimbali. Mimi pia naunga mkono hoja hii lakini pia naona kuwa haya ni matokeo zaidi ya matatizo ya ndani ya Simba ambayo naweza kudiriki kusema ni ya kujitakia.
Kwa uchunguzi wangu, Simba bado ni moja kati ya timu nzuri zilizoko katika ligi hii ya VPL lakini inakabiliwa na matatizo makubwa mawili ambayo ni ya kujitakia na hivyo yako ndani ya uwezo wao kuyasahihisha na tatizo moja dogo kama nitakavyoeleza hapa chini.
1. Kukosa mwendelezo (lacking consistence)
Imeshazungumzwa sana na hadi sasa inachosha kusema kuwa kikosi cha Simba hakina uzoefu wa kutosha kwa kuwa kinatumia wachezaji wengi vijana, lakini pia kikosi hakijazoeana tangu wachezaji hadi benchi la ufundi. Kutokana na matatizo haya yote, Simba, kwa misimu mitatu mfululizo haiianzii pale ilipoishia; ila kila msimu na kwa hakika ni kila nusu msimu (kila raundi) Simba ni kama huwa inaanza upya!!!
Kutokana na hali hii, timu haijengwi vizuri kwa maana ya kujengwa juu ya msingi hatua kwa hatua hadi kufikia ubora wa juu wa kikosi. Ndio maana Simba kupoteza wachezaji mihimili ktk kila idara ni kitu cha kawaida na hakishtui. Rejea Musoti, Tambwe, Kiemba, Chanongo, na Owino ambaye inasemekana yuko mguu ndani mguu nje. Mlundikano wa kukosa uzoefu kutokuzoena na benchi jipya kila baada ya miezi mitano ndio tatizo kubwa na la ndani kabisa la Simba
Hata matokeo ya kuchoka mapema inaweza kuwa ni matokeo ya mwalimu mpya kutohusika na maandalizi ya mwanzo wa msimu, kwa hiyo hii sio sababu ila ni matokeo.
2. Kukosa Mshikamano ndani ya Klabu na Timu
Taarifa za kutiliana mashaka baina ya mashabiki na mashabiki, mashabiki na watendaji na watendaji kwa watendaji, kushikana uchawi, kuhujumiana, n.k ni vitu vya kila siku ndani ya Simba kwa zaidi ya miaka 5 sasa. Madhara ya hali hii yako kisaikolojia zaii kwa kuwa watu na hasa wachezaji wanakuwa katika pressure kubwa muda wote na kadiri mechi inavyokuwa ngumu ndani ya uwanja ndio pressure huzidi na kivyo kuathiri performance ya wachezaji. Kila mtu ni shahidi Simba inapokuwa na umoja kama ambavyo hutokea umoja wa kinafiki wakati wa mechi za Yanga jinsi inavyokuwa hatari zaidi. Kwa lugha nyingine mapungufu mengine ktk kikosi yangeweza kuzibwa na umoja tu ndani na baina ya timu kwa kuongeza ari ya kupambana
3. Ligi ni Ngumu na Haitabiriki
Hiki ni kitu ambacho watu wengi na hususani mashabiki hawataki kukikubali kwa kuwa tunaishi katika kwa mazoea sana. Ugumu wa ligi hii hauko katika ubora wa kiwango cha uchezaji ila katika saikolojia ya kila timu kutokukubali kufungwa. Timu ziko tayari kukabana hadi shingo, kupiga viatu, kukamiana, kupoteza muda na kufanya kila lililo ndani ya uwezo kuhakikiksha inapata matokeo bila kujali ugumu wa mechi. Ni timu zinazoweza kuhimili pressure kwa ukomavu kama Yanga na Azam ndizo zinaweza kupata matokeo hata katika mazingira magumu wakati mwingine bila kujali zinachezaje. Simba si mojawapo ya timu hizo. Bado Simba inacheza mpira wake laini, pasi nyingi (sexy football) lakini inakosa plan B mambo yanapokuwa magumu.
Kwa kuhitimisha, sababu ya kwanza na ya pili iko ndani ya uwezo wa Simba na ni sababu kubwa zaidi zinazopelekea timu kupepesuka. Aveva na kamati yake wanaweza kuimaliza kabisa ndani ya miezi michache ijayo. Hii sababu ya tatu ni nje ya uwezo na kwa kweli ni changamoto kwa Simba na timu nyingine zinazofanya vibaya kujipanga kivingine ili kubaki ktk ushindani wa kweli.