Wajumbe tunaishi nao mtaani
Binafsi pia ni mjumbe wa mkutano mkuu Nina marafiki zangu zaidi ya 50 hawakubaliani na Mbowe kuendelea!!
Pia ndio tunaishi nao humu mitandaoni
Kwani wenyewe hawapo Jamiiforus, twiter na Facebook?
Ukiangalia kura ya maomi mtandaoni 98% ya maoni wanamkubali Tundu Lissu
Tusidanganyane Mbowe hawezi kufikisha hata 25% ya kura za wajumbe 1200 hata akiwahonga watakula pesa zake bure na kumpiga kura Lissu
Binafsi Nina watu zaidi ya 50 ambao Nina uhakika watampa kura Lissu na hao Wana watu tu wao.
Kama Kuna mwaka mbowe anaenda kupata aibu ni mwaka huu ujao 2025.
Kikubwa na la muhimu hapa ni kuwa, safari hii Freeman Mbowe amekumbana na kisiki...
Kama bado ana matamanio ya kuendelea kuwa top leader wa chama hiki, basi anapaswa kufanya kazi ngumu na ya ziada sana ya kujenga hoja za msingi na thabiti ili kumfanya huyu mpinzani wake kuwa irrelevant kwa wana CHADEMA na nyie wajumbe 1200....
Katika hili, sioni atajenga hoja gani ili aeleweke na kukubalika....
Nimemsikiliza jana wakati anaongea na watu wake waliomfuata nyumbani kwake kumshinikiza achukue fomu, sikupata substance ktk hotuba yake zaidi ya kupita mulemule wapambe wake walimopita. Hakuwa na hoja kabisa ya kiuchaguzi. Labda hiyo J'mosi anayosema atatoa msimamo wake...
Most importantly, sikuona hoja kama ambavyo mwenzake Tundu Lissu anaazo. Nilichokiona ni mipasho na vitimbwi vya muda wote sawasawa na wapambe wake....
Kama katika uchaguzi huu mtachagua hoja, Freeman Mbowe is completely out of time....
Hana hoja tena, hana ushawishi tena na kilichobaki ni kujisifia kuwa "amekijenga chama kwa mateso ya damu na jasho" hoja ambayo hata hajui kuwa mwenzake Tundu Lissu pengine ndiyo inamhusu zaidi kuliko yeye kwa kuwa alipigwa risasi, amefungwa na kushitakiwa mara nyingi kuliko yeye kwa sababu ya chama hikihiki...!
Na unajua ndugu
technically kuna kitu kimoja ambacho watu wengi tuliomo humu hawakioni kuhusu uchaguzi wa mweyekiti CHADEMA (T) awamu hii, ni ishu ya u - speciality wa uchaguzi huu tofauti na ule wa mwaka 2009, 2014 na 2019....
Upekee wake ni mtu aliyejitokeza kuutaka uenyekiti, Tundu Lissu tofauti na tuliyemzoea Freeman Mbowe....
Katika chaguzi zilizopita, Freeman Mbowe amegombea na wagombea dhaifu sana ambao wengi waliletwa na dola lengo likiwa ni CHADEMA kuwa na kiongozi mamluki wa CCM na serikali yake....
Tulisimama imara kumpa back up mwenyekiti Freeman Mbowe pamoja na matukano mengi juu yake na chama kwa ujumla ya kuwa "ni mroho wa madaraka na CHADEMA hakuna demokrasia". Mara zote hila hiyo ilishindwa kwa wote kusimama imara kukipigania ndani na nje ya chama....
Safari hii, tuna mgombea huru kabisa, mfia chama, asiye na uhusiano wowote na CCM na serikali yake, mtu msomi na mwenye ufahamu na uelewa wa hali ya juu wa mambo, mtu asiye mnafiki, mtu anayechukia rushwa kwa maneno na kwa vitendo, mpenda haki na utaratibu, jasiri na asiyeyumbishwa wala kutishwa na yeyote na chochote...
Huyu mtu (Tundu Lissu) anapigwa vita na pande zote. CCM na serikali yao pamoja na mamluki yao yaliyomo ndani ya CHADEMA....
CCM na serikali yake, ktk mazingira haya wanaona ni heri ya Freeman Mbowe kuliko kuwa na mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani wa sampuli ya Tundu Lissu maana ni tishio la uwepo na uhai wao. Wanaona kabisa kuwa, huyu mtu kwa ufahamu na uelewa wake wa masuala kama atautumia kuumwanga kwa wananchi nchi nzima, nchi hii haitatawalika kwa staili ya ki - CCM na hivyo maslahi ya utawala na watawala hawa wa CCM yatakuwa hatarini kutoweka...
Freeman Mbowe naye kwa upande wake na wapambe wake, wako kwenye wakati mgumu sana....
Na hapa tuseme wazi kuwa, kama Freeman Mbowe atajitosa kupambana na Makamu mwenyekiti wake kwa sababu ziwazo zozote zile, dunia nzima itajua na kutambua kuwa, kumbe huyu bwana alikuwa na ZERO SUCCESSION PLAN kwa maana kumbe hakuwa na mtu yeyote aliyemwandaa kuja kuvaa viatu vyake.....!
Well. Kama yupo, basi ni vyema akamwelekeza kuchukua fomu, ampambanie na kupigia kampeni mpaka ashinde....
Kama hayupo aliyemwandaa, basi tutamwona yeye na hii itakuwa ni ushahidi wa uthibitisho kwa upande wa pili wa udhaifu wake kiuongozi, udhaifu mbaya kabisa unaojengwa ktk msingi wa kiongozi mbinafsi na asiye na vision au mipango ya mbeleni ya kitaasisi kwa manufaa ya taasisi....
Kiongozi bora na makini wa taasisi yoyote huandaa sucession plan miaka 5 hadi 10 mbele atakapoandoka madarakani....
Sasa akiamua kugombea yeye tena, hakika atakuwa wakati mgumu sana kuliko aliowahi kuwa nao ktk maisha yake yote ya siasa za upinzani hata ikitokea ameshinda either by hooks or crooks, maana dola na chawa ndivyo wanavyodai...