Mwishokambi
JF-Expert Member
- Nov 23, 2020
- 390
- 1,425
Algeria ni nchi yenye mafanikio makubwa kisoka kama ilivyo Egypt, Morocco, na Tunisia.Ni nchi ambayo inaweza kuomba mechi ya kirafiki na Brazil ikakubaliwa bila masharti, inaweza kuomba mechi ya kirafiki na England na hata Italia au Germany na ikashinda au kutoa sare.Ina wachezaji wanaotambulika ulimwenguni akiwemo winga wa Man City, Mahrez, ina wachezaji wanaochezea vilabu vikubwa hapa afrika na ulaya, Algeria iko karibu na ulaya, ina kila facilities katika soka.
Leo imeiadhibu vikali Taifa Stars, kama ilivyofanya kwa Uganda.Kiukweli Leo Stars ingeifunga Algeria, vyombo vya habari vya kimataifa vingeweka mjadala, hata kocha wa Algeria angeweza kupoteza kazi, Stars imejitahidi sana, imepambana mno, lawama kwa kocha Kim Poulsen kuwa hakumpanga Farid Mussa, cjui Sure Boy angeanza, cjui angemtoa Mzamiru na kumuacha Fei Toto ni upopoma wa hali ya juu.