Tusiende Kwenye Uchaguzi Mkuu Pasipo Katiba Mpiya

peche luke

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2013
Posts
365
Reaction score
106
Kwa mambo yanavyoendelea sasa kuna kila uwezekano kuwa hadi 2015 tutakua hatujapata katiba. Ushauri wangu tuone uwezekano wa kuongeza muda wa uongozi tulio nao sasa mpaka tuwe na katiba itakayo ridhiwa na wote.
Angalizo muda tutakoongeza usizidi miaka mitano tu basi.
 
Hakuna kuongeza muda na lazima Katiba mpya ndani ya muda uliyopangwa, kama hayo ndiyo matarajio ya CHADEMA wamenoa.
 
Mimi nadhani hakuna haja ya kuongeza muda kwa utawala uliopo. Ikishindikana kabisa kukamilisha katiba mpya basi yafanyike mabadiliko kwenye katiba ya sasa kuunda tume huru ya uchaguzi na kuweka misingi ya uchaguzi huru na wa haki ili tupate uongozi mpya wa kidemokrasia utakaoendeleza gurudumu la kuandika katiba mpya..
 
Lazma tuwe na katba mpya on time,na uchaguz 2015 bila katiba mpya hautokuwa na tofaut na ule wa 2010,so katib mpya inaitajika il mabadiliko yawepo
 
Kwa mambo yanavyoendelea sasa kuna kila uwezekano kuwa hadi 2015 tutakua hatujapata katiba. Ushauri wangu tuone uwezekano wa kuongeza muda wa uongozi tulio nao sasa mpaka tuwe na katiba itakayo ridhiwa na wote.
Angalizo muda tutakoongeza usizidi miaka mitano tu basi.
kaka naona unataka kumalizia na kibanda chako cha 10 nini?,
 
Kwa mambo yanavyoendelea sasa kuna kila uwezekano kuwa hadi 2015 tutakua hatujapata katiba. Ushauri wangu tuone uwezekano wa kuongeza muda wa uongozi tulio nao sasa mpaka tuwe na katiba itakayo ridhiwa na wote.
Angalizo muda tutakoongeza usizidi miaka mitano tu basi.

......pia si busara kuharakisha kupata katiba mpya kwa ajili ya general election ya 2015. Lakini pia kufanya general election 2015 kwa katiba ya sasa ni maafa. Ni bora kuwe na interim government baada ya muda wa serikali ya sasa ili tuendelee kutengeneza katiba bora yenye maridhiano ya kitaifa. Hatuna budi kuchagua njia njema yenye maslahi mapana kwa taifa.
 
Hapo kwenye interim govermemt naomba kutofautiana na wewe. Tuendelee na waliokuwepo kwani wanaouzoefu. Tusisahau utashi binafsi wa mheshimiwa kuhusu katiba. Hiyo interim goverment itakuwa kujichanganya tu.
 
Kwa mambo yanavyoendelea sasa kuna kila uwezekano kuwa hadi 2015 tutakua hatujapata katiba. Ushauri wangu tuone uwezekano wa kuongeza muda wa uongozi tulio nao sasa mpaka tuwe na katiba itakayo ridhiwa na wote.
Angalizo muda tutakoongeza usizidi miaka mitano tu basi.

Hiyo miaka mitano ni term nzima ya uongozi. Siungi mkono hoja kwa sababu watawala wataendelea ku delay mchakato wa katiba ili waendelee kutawala. Uchaguzi ufanyike kama kawaida. Na wao kuendelea kutawala bila uchaguzi ni kwenda kinyume na katiba ya sasa ambayo bado iko valid mpaka hapo katiba mpya itakapopitishwa.
 
Well said andate, ndugu yetu peche luke anasahau kuwa wanasiasa na madaraka ni kama samaki na maji.

Mbaya zaidi ndugu yetu anasimamia katika "utashi binafsi" wa mtu mmoja tu huku hali ikizidi kuthibitika kuwa chama dola hakina huo utashi wa dhati katika kupata katiba inayokidhi maslahi bora ya taifa kwa leo na miaka hata 100 ijayo.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom