Sister Abigail
JF-Expert Member
- Sep 2, 2020
- 2,886
- 9,088
Tusilete ushabiki kama ule wa SIMBA na YANGA linapokuja suala la uchaguzi, tukiitana majina sijui nyumbu sijui mataga, hii ni hatma yetu ni maamuzi kwa faida yetu ya kesho. Likitokea baya tutalibeba wenyewe, na likitokea zuri tutafaidika nalo wenyewe kama Watanzania. Huu sio Mpira tuseme wamemaliza fulani kafungwa, fulani kashinda bhasi maisha yataendelea.
Hapana huu ni uchaguzi wa kuamua tunataka tuishije huko mbele miaka mitano ijayo, hatma yetu kama Watanzania.
Kuna maisha baada ya uchaguzi, na maisha tunayotaka yataamuliwa na sisi wananchi kupitia sanduku la kura.
Ombo langu tuache mihemko,tutumie akilii kujua ni mgombea yupo atakaetufaa.
Hebu fikiri A anamdiss B kwenye jukwaa, ohh yule ni kibaraka katumwa kuja kuvuruga amani, atawavuruga atawaacha peke yenu, ila cha kushangaza sasa yeye huyohuyo anaejitapa mzalendo MTU wa amani anamshambulia kwa mabomu yule anaemtaja kuwa kama mvuruga amani, inaingia akilini kweli?
Mtu anaonesha dhahiri kabisa ni muonevu wa kila aina,bado mnamshangilia hizi ni akili au mihemko? Kama ameweza kuwaonea hao atashindwa kukuonea wewe?
SERIKALI NI MFUMO WA WATU, ULIOUNDWA NA WATU KWA AJILI YA WATU
Na watu hao ni sisi wanachi, Watanzania Sisi ndo tunaowapa dhamana ya kutuongoza,na sisi ndo wa kuamua tuongozwe na MTU wa aina gani?
Maamuzi yapo kwetu. Na maisha yatayokuja chini ya huyo tuliemchagua ni yetu, kama mnyanyasaji tutanyanyasika sie, kama muonevu tutaonewa sie, kama ni muuwaji tutauliwa sie, kama ni mdhulumu tutadhulumiwa sie, vitisho sisi, kuburuzwa na kutupwa gerezani sisi, kufilisiwa Mali zetu sisi, kutekwa sisi, kunyimwa ajira sisi, kuuliwa biashara zetu kimabavu sisi, kukatwa kodi kandamizi sisi.
Wakulima wataoteseka ni Watanzania
Wafanyabiashara ni Watanzania
Walimu ni Watanzania
Wafanyakazi ni Watanzania
Wanafunzi ni Watanzania
Sio Kenya, Uganda wala Burundi. Ni Tanzanians!
Uchaguzi huu ni maamuzi ya kutaka tuishije tena awamu ijayo. Tusiwe wepesi kutumia AKILI.
Tuache MIHEMKO tutumie AKILI kuchagua kilicho bora kwa faida yetu wenyewe!
Mungu Ibariki Tanzania.
Abigail Nabal