wabunge gani hao ulio na imani nao? Ni hao wa ccm ambao wengi wao ubunge wameupata baada ya uchakachuaji wa kura? Nakubaliana na mtoa hoja, kwamba kuna umuhimu wa kuhamasisha wananchi ili achaguliwe spika mwenye nia njema na muelekeo wa nchi hii na si "kibaraka" wa chama tawala. Wengi tunafahamu jinsi mhe sitta (ccm) alivyoweka hatarini nafasi yake katika chama, kwa uendeshaji wake mzuri wa bunge, na faida yake leo hii wapinzani tunaiona. Sitoshangaa kama vigogo wa ccm wakimuweka "kibaraka" ambaye atakuwa akifuata maelekezo ya chama badala ya matakwa ya wananchi.
Jamani, kuna umuhimu wa kuhamasishana na hili jambo la spika wa bunge lina umuhimu wake, kwani hata katika uchaguzi wa rais kanuni za kufuatwa zilikuwepo, na uchakachuaji ukafanyika, leo hii iweje tuseme hayo matunda ya uchakachuaji, yatafuata kanuni yatakapofika bungeni? Tusipokuwa makini nguvu zetu zitapotea bure.