SoC02 Tusiilaumu Serikali kwa vitu ambavyo sisi wenyewe vimetushinda(unafiki juu ya uhaba wa ajira)

SoC02 Tusiilaumu Serikali kwa vitu ambavyo sisi wenyewe vimetushinda(unafiki juu ya uhaba wa ajira)

Stories of Change - 2022 Competition

ONESMO MWAKAJILA

New Member
Joined
Jan 24, 2021
Posts
4
Reaction score
1
Habarini ndugu zangu wanajamii forum leo kwa mara ya kwanza naandika katika "stories of change 2022" , kwasababu ni mshiriki mgeni na Sina uzoefu wowote Wa kuandika machapisho katika hili jukwaa ,lakini ni mfuatiliaji tu wa mijadala ya jamii forum kwa miaka kadhaa ,hivyo basi nami ningependa niweze kushiriki kwa uchache katika kujenga taifa langu, hata kama sitashinda ila niseme tu mawazo yangu kwa jamii yangu, kwasababu nadhani lengo kuu la waanzilishi Wa jukwaa siyo tu kupata washindi na kugawa zawadi bali nadhani lengo ni kutatua changamoto zinazoisibu jamii hata kama si kwa alama zilizowekwa , kwasababu kinachotafutwa ni jamii nzima kushinda ,wala si watu hawa 20 tu kushinda .Najua kabisa nimeandika haya maelezo ya mwanzo kwa kukosea kwa makusudi kwasababu hayaendani na kichwa Cha habari ila nilitaka nizibe mwanya wa kuzua maswali mengi kwa watakaoniona mshamba wa kuandika ,mimi siyo mzoefu ni "Learner" ,hivyo usinicheke.

Tumekuwa na Tanzania yenye kilio kikuu kilichoenea ndani ya mipaka yake yote kuhusiana na janga la kutoajiriwa kwa wahitimu ,na wasomi tumekuwa watu wa kulalamikia serikali wakati wote kuwa haitoi ajira kwa watu wake au inaajiri wachache ukilinganisha na idadi ya wahitimu na ikiajiri basi ni kwa kubebana kindugu ,alimaarufu kama "connection" .Nilichokigundua Mimi ,ni kwamba Watanzania tunapenda kupoteza muda pasipo na sababu ya msingi ,sisi badala ya kuhangaika kutumia elimu tuliyoipata kuisaidia serikali kutatua changamoto kwa kuleta ubunifu au kuongeza ufanisi katika kutatua au kupunguza changamoto zinazolikumba taifa ,ikiwemo ajira ,tunajikuta muda wote tumebaki kulaumu serikali na hatima yake ,tunajikuta hakuna tunachobadilisha bali kuzidi tu kujichelewesha zaidi na kujenga chuki juu ya serikali na waajiriwa wake.

Mimi kama nilivyosema sitaandika maudhui haya kwa ufundi bali nitaelimisha kwa nitakapoweza kuishia sawasawa na ufahamu nilionao , kwasababu siwezi nikafanya zaidi ya ufahamu wangu ,hivyo nitakavyoandika iwe kwa kukosea au kupatia hapo ndipo ufahamu wangu ulipoishia na nitaandika kile ninachokiishi kwa uhalisia wangu .Mimi ni miongoni mwa wahitimu wasio na ajira ,nimesoma shahada ya kwanza ya sayansi katika uhandisi wa kompyuta katika chuo kikuu Cha sayansi na teknolojia cha Mbeya ,lakini moja ya kitu nilichozuia akili yangu isishughulike nacho kabisa Wala kuhangaika nacho ni kulalamikia serikali juu ya ajira ,kwakuwa kwanza naelewa janga hili siyo la kumlalamikia mmoja au wawili ninaowaita viongozi au waajiri bali ,hili ni la kitaifa/ kiserikali ambapo Mimi mwenyewe ni mmoja wa wanaserikali au wanataifa hivyo kumlaumu mwingine ni kujilaumu mimi mwenyewe kwa kushindwa kujiendesha iwe kwa kujua/kutokujua.

Watanzania tufike mahala Mungu atusaidie kutupa ufahamu kuwa tuachane na lawama ambazo hazina suluhu badala yake tuzidi kutoa hoja na maoni yenye tija na siyo maoni pweke/tupu ,hapo tutazua tu ubishi na ushindani usio na msingi ,bali tutoe hoja zitakazoambatana na mfano halisia wa namna mtoa maoni/hoja anavyoishi au kutenda Ili kukabiliana na janga hili ,kwa mfano mtoa hoja akitaka achangie kuhusu changamoto zinazojitokeza katika kukosekana kwa soko la uhakika la Mafuta ya mawese ,ahakikishe mtu huyu yeye ni mtu anayefanya hiyo biashara au aliwahi kufanya kwa angalau mwaka mmoja biashara hiyo na siyo tu kufanya/kuwahi kufanya bali kuwe ni kufanya kulikojikita zaidi katika kutatua changamoto hizo na utuoneshe ulifikia wapi na ulifanyafanyaje ,siyo utuambie ulisikia kwa fulani akilalamikia hilo ,wahenga walisema "utamu wa ngoma ,ingia ucheze" .Wakiwa na maana kwamba huwezi ukaona au kung'amua uhalisia wa jambo bila kulisogelea kwa ukaribu na pia kuligusa/kulishika ,ndiyo maana mpishi mzuri kabisa lasima aonje mboga kama imekolea chumvi ,hatumii macho ,masikio na pua pekee .Kusema hivi siyo kwamba nakataza watu wasitoe maoni kwa kitu ambacho hawajawahi kukifanyia kazi kwa vitendo bali nilikuwa nashauri jamii kuwa ,kwa uzoefu wangu ,asilimia kubwa ya wakosoaji/walalamishi au watoa maoni mitandaoni /serikalini ni watu wenye hoja pweke zilizokosa udadisi wa kina juu ya kitu wanachokitolea maoni ,hivyo wanajikuta wanazua tu ubishi na kulalamikia viongozi kwa lawama ambazo haziwezi kuleta mageuzi yoyote kwasababu hazina utafiti na uthabiti na mara nyingi huchukuliwa kama kelele tu zinazopelekea chuki na hila juu ya serikali.

Ukiachana na elimu yangu ,Mimi pia ni Moja ya wanafunzi niliyepambana Sana na biashara ndogondogo ili nipate angalau mahitaji kidogo ya shuleni ,mwaka 2012 nikiwa kidato Cha kwanza niliwahi kufungua kituo kidogo Cha kuoshea magari ,lakini nikashindwa kukiendeleza kwasababu ya kukosa muda wa kuendesha hiyo kazi na masomo ,pia kutokana na miundombinu hafifu niliyokuwa nikitumia ,niliuza karanga na vimaandazi vya ndizi na unga (vibama),na niliuza pipi hadi nilipohitimu kidato Cha nne 2015 ,nilipofika kidato Cha tano na sita niliuza chipsi kwa kuajiriwa ,nilipofika chuo kikuu ndipo nilitanua wigo kidogo ,nilifanya biashara ya samaki mtera ,nimefanya kazi za kubeba mizigo kwa matajiri (cargo),nilifanya biashara ya Kakao ,niliuza matunda ya matufaa (apples) ,niliuza viatu vya mtumba na nilifungua mgahawa , kwasasa hizi biashara zote niliacha kuzifanya baada ya kuhitimu chuo kikuu , kwasababu nilikuwa nazifanya ili nipate kukidhi mahitaji yangu ya chuoni au shuleni wakati huo ,lakini huku nikitafuta kupata uelekeo sahihi wa maisha kwa kujiajiri na nimezijua changamoto zinazojitokeza katika shughuli hizi na mpaka nimehitimu Sasa nipo mtaani ,napambana na biashara ya kuuza Mafuta ya mawese hapa Wilayani Kyela.

Jitihada zote hizi na kufurukuta huku kumenifanya kuwa mtu ninayejua uhalisia wa changamoto katika shughuli nyingi za kiuchumi na ndiyo maana Mimi najiona angalau naweza kutoa maoni yenye maana kidogo kwa serikali juu ya biashara hizi kwasababu nazijua changamoto kwa uhalisia wake ,na ndiyo maana pia hutakuja kunikuta nailamu serikali kwa kutotoa ajira kwa watu , kwasababu najua changamoto zilizonifanya Mimi kutofikia hatima za biashara hizo ,zinanipa picha kuwa kama Mimi mwenyewe yalinishinda basi ndiyo maana pia serikali nayo kwa viwango vyake inashindwa kufika malengo yake kwa kukutana na changamoto za hadhi yake vilevile ,hivyo wajibu wangu Mimi niendelee kupambana kutafuta suluhu na nisimpambananishe mtu na changamoto ambayo Mimi mwenyewe imenishinda ,kama ni kushauri nishauri kwa jambo nililoliweza na nileleze niliwezaje .


Hivyo kwa kumaliza niseme kwamba Watanzania tutoe hoja za msingi zitakazoleta suluhisho ,siyo kulaumu serikali kwa kitu ambacho hatujakifanyia udadisi yakinifu na hatujawahi kukijaribu na kukifanya kwa uhalisia wake ,tuachane na hisia kuilaumu serikali , kwasababu sisi wenyewe tunaolalamika ndiyo serikali hiyohiyo. Kama wewe mwenyewe una kampuni ndogo au kiwanda kidogo na umeshindwa kuajiri kijana hata mmoja au wawili kwa ubahili wako, halafu unakuwa wa kwanza kulaumu serikali kuwa haiajiri watu ,ni kiwango Cha juu Sana Cha ukorofi na ubishi ,wewe pia ni serikali kama umeshindwa kuajiri hapo kwako ,basi usiilaumu serikali, unapata kila mwezi milioni Moja ,inakuuma kumuajiri kijana unayeweza kumpa walau elfu 40000 kwa mwezi, tuacheni ujinga na hila juu ya serikali Watanzania ,tusiilaumu serikali kwa kitu ambacho sisi wenyewe kimetushinda, Mimi nimemaliza.

FB_IMG_1662956051466.jpg
 
Upvote 1
Back
Top Bottom