TUSIJIDANGANYE NA KILIMO: Tunachumia tumbo tu ila kwa kimataifa tumeachwa mbali sana

TUSIJIDANGANYE NA KILIMO: Tunachumia tumbo tu ila kwa kimataifa tumeachwa mbali sana

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,958
Reaction score
3,890
Iliobaki ni kudanganyana na kuibiana yaani hakuna faida hata ya kuwa na waziri wa kilimo,wa nini? hana jipya wala uwezo wa kutufanyia lolote, kama ni mbio tumeshapitwa na tumeshachoka utampitaje alie kupita?

Mazao yetu hayana kiwango cha kuuzwa nchi zanje kwa sababu wizara ya Kilimo wao ni kugawa mbegu na wenyewe wanaona wamefanya au wanafanya jambo kuuuuuuwbwa, ni sifuri wafunge wizara kwa kilimo cha kula wenyewe hatuhitaji mabwana shamba koko wachumia matumbo yao.

Machungwa yanatuozea, mananasi yanatuozea yaani matunda kibao yanatuozea mashambani na mikononi, wizara haina mikakati ya kusababisha bidhaa kusafirishwa majuu na uwekezaji tulionao ni sifuri,

Ndugu zanguni ingieni kwenye guguli muangalie matunda yanavyotayarishwa na kuweza kufikia kiwango cha kukubalika, mashamba ya minanasi huoni mwisho, mashamba ya miembe utadhani shamba la mkonge miembe ilivyopangana huoni mwisho, watu wanavuna kwa mashine, michungwa, migomba.

Sasa kama haitoshi kutoka shambani tunda hupelekwa kwenye usafi wa kulisafisha tunda na kufuatiliwa na packing and packaging, hapa kwetu likitoka shambani limesafiri limefika chalinze kwa mlaji, chungwa linafika hadi south Sudani sisi hufikisha Kenya Wakenya husonga zaidi. Kenya wakifunga mipaka bidhaa zinaoza kwenye malori.

Hizi TV zetu zituonyeshe vilimo vya kisasa wachukue hata video za youtube wazirushe zitatusaidia kupanua wigo wa mawazo na kachana na hawa mawaziri wajaza baraza.
 
Naupenda ujamaa ila nao una madhara yake kama haya. Wewe unataka serikali ya nchi kama hii iwekeze vipi kirahisi zaidi ya vile inavyofanya sasa? Serikali kila uchao inajenga miundombinu itayowezesha usafirishaji rahisi na wa gharama nafuu kuyafikia hayo masoko uyasemayo.

Inajenga cold rooms kwenye airports, inanunua ndege, inajenga railway stations zenye cold rooms, imeagiza mpaka mabehewa ya baridi!

Wewe mjamaa umekaa hapo nyuma ya keyboard unalalama matunda yanaoza! Unataka serikali ije ikwambie "sasa chuma hili limeiva, lile chuma kesho!". Makampuni na taasisi zilizobobea kuuza bidhaa zao nje ya nchi changamoto yao kubwa ni uzalishaji mdogo kuliko ukubwa wa soko huko nje!

Tuache kufikiri kama vile tuko kwenye zile zama za ujamaa. Sasa ni dunia ya kisasa, yapasa kufikiria kijasiriamali zaidi. Nenda pale TAHA waulize kuhusu standard zinazotakiwa kisha pambana uzifikie.

Stop complaining and making excuses, plan.
 
Siandiki mengi ila kwa Afrika ya Mashariki na kati shamba ni Tanzania na wanaolima ni hao ndugu zetu vijijini ambao ni small peasants na hawathaminiki.

Kenya machungwa anaagizia kwa asilimia kubwa Mkoa wa Tanga ina maana horohoro pakipigwa pini wao hawana uzalishaji mkubwa watapotea,ukigusia mazao ya nafaka nenda Congo na Zambia utaelewa hata hao kenya pia sijataja Komoro hapa na viinchi vingine.

Sera yetu labda iwekwe sawa mkulima afaidike japo mwangaza kama mambo yakikaa sawa tutauona maana hata ishu za Exportation tunajaribu taratibu tunawahama Kenya japo taratibu kwa hapa kwetu ni ndefu ziangaliwe kwa upana kusaidia wakulima na mifumo kama Cold rooms iwekwe zile hot centres kama walivyofanya Njombe.
 
Back
Top Bottom