Rashda Zunde
JF-Expert Member
- May 28, 2022
- 204
- 231
Ni vyema kutambua kuwa suala la sensa ya watu na makazi halifanyiki kwa manufaa na maslahi ya chama, dini wala kabila bali linafanyika kuisaidia serikali kupanga mipango yenye tija kwa kila Mtanzania.
Ukirejea umuhimu wa sensa ya watu na makazi, sioni kama kuna sababu yoyote ya msingi itakayomfanya mtu asiweze kushiriki ama asiwe tayari kutoa taarifa zake na kama yupo basi huyo ni msaliti naye anapaswa kutafakari maamuzi yake kwa maslahi yake binafsi na ya nchi.
Ni lazima tujiweke tayari kuhesabiwa na ili tufanikishe hili ni vyema tukemee, tukatae na kukanusha taarifa zenye kutia doa na kizuizi ushiriki wetu katika sensa kwani kutoshiriki sensa ni mithili ya usaliti.
Hata Rais Samia Suluhu wakati akizindua rasmi nembo ya sensa ya mwaka 2022 aliwaomba Watanzania wote kujizatiti na kujiweka tayari kushiriki sensa.