Tusijisahaulishe hii nchi ni yetu sote

hitler2006

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2014
Posts
489
Reaction score
454
Kuna namna ambayo inashangaza kadiri siku zinazovosonga mbele,kwa wafuatiliaji wa mambo tunaona namna ambavyo baadhi yetu(watanzania) waliokatika nafasi mbalimbali wanasahau kuwa wao ni sehemu ya jamii na lolote linalowasibu wanajamii kwa namna yoyote ile litawagusa kwa namna moja ama nyingine hivo hawana budi kufuata taratibu na sheria tulizokubalia kama jamii ya watanzania huru na wenye akili timamu...

Kuna watu wamesahau kuwa mamlaka hutoka kwa wananchi na wao wamekasimishwa iko siku hawatakua tena kwenye viti vya maamuzi na watakua wahanga wa maamuzi yao ya sasa, kama si wao basi "vizazi vyao labda kama ni matasa na hawazai"

Lakini pia kuna wale wambao kila uchwao hawachoki kutoa maneno yenye ukakasi na viashiria vya kuleta sintofahamu katika jamii, tuwakumbushe tu...pakiharibika hapa hatuna pakwenda wengi wetu, maana hata pasipoti hatuna...

KILA MMOJA WETU ATIMIZE WAJIBU WAKE MAHALI ALIPO, AMANI HAINA MBADALA"

Bila kusahau amani ni zao la haki

Pia soma:Kwa tulipofikia ni bora serikali yote ijiuzulu na uitishwe uchaguzi kabla ya 2025 ili kupata serikali itayoipelekea nchi yetu mahali sahihi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…