Ndugu yangu Pundamilia.
Tangu watanzania tumepata uhuru wa kuona ligi za mpira za wenzetu na maendeleo ya TV kufika vijijni wengi wetu tumepunguza ushabiki wa simba na yanga na wengi tuna hata ile courage ya kusema "kweli tumefungwa na timu yetu ilicheza vibaya" jambo ambalo enzi za nyuma ilikuwa si rahisi kulisikia.
Katika siasa vile vile,binafsi nimebafatika kuisoma report ya kitengo cha makosa makubwa ya rushwa kilichochunguza siuala la Chenge.Naamini kwa utawala wa sheria pamoja na kuwa ni tuhuma huyu angekaa pembeni na labda asingesafishwa na akarudi akiwa clean kuliko ktembeza bendera ya CCM akiwa ana zimwi la rushwa mgongoni.
Ni kweli CCM inaweza ikashinda kwa kishindo lakini hilo halikuzuii kukemea mambo maovu yaliyoko ndani ya CCM ikiwemo kuwakumbatia wezi as if nchi haina watu wengine wenye ujuzi na elimu ya kutosha.
Tukubaliane kuwa hata ukiwa mshabiki wa CCM ifike mahali useme "hapa tumechemsha".