Ni muhimu taifa kuanzisha kampeni ya mapema ya kuwakataa vibaraka wa mabwenyenye ya magharibi kwenye sanduku la kura 2030

Ni muhimu taifa kuanzisha kampeni ya mapema ya kuwakataa vibaraka wa mabwenyenye ya magharibi kwenye sanduku la kura 2030

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
51,453
Reaction score
41,274
Hii itachochea kwa kiasi kikubwa ari ya uzalendo miongoni mwa wananchi, na kuweka maslahi mapana ya waTanzania wote mbele kuliko maslahi binafsi.

Kwakuwa vibaraka wa mabwenyenye ya magharibi nchini wameshajibainisha wenyewe, ni jukumu letu sasa kama waTanzania kuchukua hatua muafaka za makusudi kabisa, ikiwa ni pamoja na kampeni kabambe ya kuwakataa vibaraka na mamluki wao nchini.

# Kataa vibaraka wa mabwenyenye ya magharibi kwenye sanduku la kura uchaguzi mkuu 2030.🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Hii itachochea kwa kiasi kikubwa ari ya uzalendo miongoni mwa wananchi, na kuweka maslahi mapana ya waTanzania wote mbele kuliko maslahi binafsi.

Kwakua vibaraka wa mabwenyenye ya magharibi nchini wameshajibainisha wenyewe, ni jukumu letu sasa kama waTanzania kuchukua hatua muafaka za makusudi kabisa, ikiwa ni pamoja na kampeni kabambe ya kuwakataa vibaraka na mamluki wao nchini.

# Kataa vibaraka wa mabwenyenye ya magharibi kwenye sanduku la kura uchaguzi mkuu 2030.🐒

Mungu Ibariki Tanzania
Naunga mkono hoja asilimia 100% kwa 100%,
Ni kweli hao vibaraka wapo, na hatua ya kwanza ni kuwabaini, kuwatambua, kuwataja tuwajue na tuwaangamize kabla ya 2030!,

Ile siku kiongozi mmoja alipowataja vibaraka wapumbavu, nilimuunga mkono na nikatoa ushauri PNA: Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba ni Mkweli Kama Nyerere, Namuunga Mkono Kauli ya Vibaraka Wapumbavu, Tusiishie Kuwasema Tuu, Je Tuwataje Tuwajue Au?

Ile siku waziri wangu amesema kuna watu wanamuhujumu Rais Samia kuhusu 2030, nilishauri Makonda, Kumbe kuna Watu wanapanga Njama za Kuharibu na Kudhoofisha jitihada za Rais Samia katika uongozi wake kwa Ndoto za 2030? Ni kina nani hao?

Na juzi Mhe. Simai alipomtaja Yuda Bungeni, nilimuunga mkono na nikashauri PNA: Tuheshimu Mawazo ya Wengine Hata Kama Hukubaliani Nayo!, Simai ni Jasiri, Shujaa, Hoja ya Yuda ni ya Msingi, Asibezwe, Asikilizwe Afafanue!.

Tuwataje hao vibaraka wapumbavu, hao wahujumu na wasaliti tuwajue tuwashughulikie,

P.

P
 
Hii itachochea kwa kiasi kikubwa ari ya uzalendo miongoni mwa wananchi, na kuweka maslahi mapana ya waTanzania wote mbele kuliko maslahi binafsi.

Kwakua vibaraka wa mabwenyenye ya magharibi nchini wameshajibainisha wenyewe, ni jukumu letu sasa kama waTanzania kuchukua hatua muafaka za makusudi kabisa, ikiwa ni pamoja na kampeni kabambe ya kuwakataa vibaraka na mamluki wao nchini.

# Kataa vibaraka wa mabwenyenye ya magharibi kwenye sanduku la kura uchaguzi mkuu 2030.🐒

Mungu Ibariki Tanzania

Mimi binafsi nimechagua upande ule ambao dhamira yangu inanionyesha, bila upendeleo wala dharau.

Haya maneno yako unaongea leo wakati tumeshatengeneza matatizo mengi ambayo yangeweza kuepukika. Ngoja tuendelee na safari ili hatimaye tufike kule ambako kwa ubabe tumeamua twende.

Kwenye hali kama hizi, mabepari wanapenda sana, maana kuna migawanyiko. Tukumbuke, mabepari wanapenda kusema, A house divided against itself cannot stand.
 
Hii itachochea kwa kiasi kikubwa ari ya uzalendo miongoni mwa wananchi,
Wacha hadaa
Chawa wa watawala haramu hawezi kuwa mzalendo, bali ni msaliti wa taifa..

Naunga mkono hoja asilimia 100% kwa 100%,
Ni kweli hao vibaraka wapo, na hatua ya kwanza ni kuwabaini, kuwatambua, kuwataja tuwajue na tuwaangamize kabla ya 2030!,
Mtawaangamiza vipi, kuwateka na kuwauwa?
 
Hili ni bandiko la PETER MSIGWA huko X, na copy na ku paste hapa kwa ajili ya wale ambao hawaingii kule X..
👇

KATIKA DEMOKRASIA:
Mahakama ni kubwa kuliko Jaji Mkuu.
Bunge ni kubwa kuliko Spika.
Taifa ni kubwa kuliko Rais.
Katiba ni kubwa kuliko chama tawala.

Hii ni kwa sababu taasisi zinapaswa kudumu, wakati viongozi ni wa muda.

1. TAIFA NI KUBWA KULIKO RAIS
Rais ni kiongozi wa muda.
Taifa ni la kudumu.
Rais anaweza kukaa madarakani miaka 5, 10 au 20.
Lakini taifa linaendelea kuwepo kabla yake na baada yake.

Mfano:
United States imekuwa na marais wengi sana.
Wamekuja:
Ronald Reagan
Bill Clinton
Barack Obama
Donald Trump
Lakini Marekani imebaki kuwa Marekani.

Rais ni mtumishi wa taifa.
Taifa si mali ya Rais.
Ndiyo maana katika demokrasia, kumpinga Rais si sawa na kulichukia taifa.

Na kumuunga mkono Rais si sawa na kuwa mzalendo.
Uzalendo ni kuipenda nchi hata pale unapokosoa serikali.

2. SERIKALI SI TAIFA
Hili ndilo eneo ambalo watu wengi huchanganyikiwa.
Serikali ni chombo kinachosimamia nchi kwa kipindi fulani.

Taifa ni wananchi wote pamoja na historia, ardhi, taasisi na mustakabali wao.
Kwa mfano:
Leo serikali inaweza kubadilika.
Lakini:
Tanzania inabaki Tanzania.
Bendera inabaki ile ile.
Wananchi wanabaki wale wale.
Historia inabaki ile ile.
Kwa hiyo:

Kuikosoa serikali si kuisaliti nchi.
Na:
Kuisifu serikali si lazima iwe kuipenda nchi.

Swali muhimu ni:
“Je jambo hili linafaidisha taifa?”
si “Je jambo hili linaifurahisha serikali?”

3. CHAMA TAWALA SI SAWA NA NCHI
Hili ni somo muhimu sana kwa Afrika.
Katika demokrasia:
Chama tawala ni mshindi wa uchaguzi.
Hakimiliki taifa. Hakimiliki serikali milele.
Hakimiliki uzalendo.

Taifa ni mali ya:
waliokichagua chama tawala,
wasiokichagua chama tawala,
na hata wale ambao hawakupiga kura.
Ndiyo maana katika nchi zilizoendelea kisiasa:
Ukikosoa chama tawala huonekani adui wa taifa.
Unaonekana sehemu ya demokrasia.

Tatizo linaanza pale chama tawala kinapoanza kuonekana kama taifa lenyewe. Hapo demokrasia huanza kudhoofika.

4. KATIBA NI KUBWA KULIKO CHAMA TAWALA
Katiba ndiyo mkataba mkuu wa taifa.
Katiba ndiyo inayotoa mamlaka kwa:
Rais, Bunge Mahakama.

Sio Rais anayeipa Katiba nguvu.
Ni Katiba ndiyo inayompa Rais nguvu.
Sio chama tawala kinachounda taifa.
Ni Katiba ndiyo inayoweka sheria za namna taifa litakavyoendeshwa.

Katika demokrasia iliyokomaa:
Kama chama tawala kinataka jambo ambalo Katiba hairuhusu,
Katiba ndiyo hushinda.

Kwa sababu Katiba inawakilisha taifa lote.
Chama kinawakilisha wanachama wake.

5. BUNGE NI KUBWA KULIKO SPIKA
Spika ni kiongozi wa muda.
Lakini Bunge ni taasisi ya kudumu.
Leo kuna Spika mmoja.
Kesho atakuwepo mwingine.
Lakini Bunge linaendelea kuwepo.
Hii ndiyo sababu taasisi ni muhimu kuliko watu.
Mtu anaweza kuondoka.
Taasisi inapaswa kubaki imara.

6. MAHAKAMA NI KUBWA KULIKO JAJI MKUU
Jaji Mkuu ni mtumishi wa Mahakama.
Sio Mahakama mali ya Jaji Mkuu.
Kesho Jaji Mkuu akistaafu:
Mahakama inaendelea.
Hii ndiyo maana ya utawala wa sheria.
Sheria inapaswa kuwa kubwa kuliko watu wanaozisimamia.

TATIZO KUBWA AFRIKA
Katika nchi nyingi za Afrika watu hufikiri hivi:
Chama = Taifa
Serikali = Taifa
Rais = Taifa
Kukosoa Serikali = Kuisaliti nchi

Hiyo ndiyo sababu mjadala wa kisiasa huwa mgumu.
Kwa sababu watu wanafikiri wanalinda taifa wakati mara nyingi wanakuwa wanalinda serikali au chama.

Lakini katika demokrasia yenye afya:
Taifa ni kubwa kuliko serikali.
Serikali ni kubwa kuliko chama.
Katiba ni kubwa kuliko serikali.
Sheria ni kubwa kuliko viongozi.
Dhamira ni kubwa kuliko utii wa kipofu.

Kwa lugha rahisi sana
Ukiniuliza tofauti kati ya nchi, taifa na serikali ningesema:
Nchi ni ardhi, mipaka na mamlaka yake.
Taifa ni watu wake, historia yao, utamaduni wao, taasisi zao na mustakabali wao.
Serikali ni timu ya muda iliyopewa jukumu la kuendesha taifa kwa kipindi fulani.

Ndiyo maana unaweza kubadilisha serikali bila kubadilisha taifa.
Lakini ukiharibu taifa, hata serikali nzuri haiwezi kulirudisha kwa urahisi.
Kwa hiyo kiongozi wa kweli hapaswi kuuliza:
“Je hili linaisaidia serikali?”
Bali: “Je hili linaimarisha taifa, taasisi zake, na vizazi vijavyo?
 
Gentleman,
ni Msigwa huyu huyu wa chadema, ambae aliondoka chadema na kujiunga na CCM akiwa na viatu vilevile, na akaondoka CCM kurudi chadema tena akiwa na viatu vilevile 🤣

unadhani akili yake itakua umebadilika sasa?🐒
 
Kuhusu hulka na misimamo yake sijui, ila ukweli usemwe, ametema MADINI ya maana, siyo kama utumbo unaoweka wewe humu kila dakika gentleman
 
Naunga mkono hoja,mabwanyenye ambayo ndiyo watu fulani yanadhania ndiyo msaada kwao,ndiyo watu hatari sana kwa dunia yetu,wao ndiyo wajenzi wa maradhi mbalimbali duniani,istoshe wanaona kasi ni ndogo wanalazimisha ushoga ili yale maradhi waliyoyatengeneza yawaingie watu vizuri sana,hawa siyo watu wema,twendeni na mzee wa 50/50 yaani russia na tutafika mbali sana,mabeberu yamekuwa waizi sana wao wanachukuwa 95 wanakupa 5.,(choice is yours)
 
Kuhusu hulka na misimamo yake sijui, ila ukweli usemwe, ametema MADINI ya maana, siyo kama utumbo unaoweka wewe humu kila dakika gentleman
mtu wa aina hiyo anawezaje kusema ukweli gentleman?🤣

wanaoweza kumuamini au kumzingatia ni lazima wawe wanafiki kama yeye alivyo tu na si vinginevyo 🐒
 
Naunga mkono hoja,mabwanyenye ambayo ndiyo watu fulani yanadhania ndiyo msaada kwao,ndiyo watu hatari sana kwa dunia yetu,wao ndiyo wajenzi wa maradhi mbalimbali duniani,istoshe wanaona kasi ni ndogo wanalazimisha ushoga ili yale maradhi waliyoyatengeneza yawaingie watu vizuri sana,hawa siyo watu wema,twendeni na mzee wa 50/50 yaani russia na tutafika mbali sana,mabeberu yamekuwa waizi sana wao wanachukuwa 95 wanakupa 5.,(choice is yours)
pamoja sana 👊
 
Wezi wa kura bwana
Gentleman,
kwa hali ilivyo,
bora wasusie tena uchaguzi,
but nadhani 2030 vibaraka watakataliwa na wananchi kwa uhuru, uwazi na haki kabisa.

itakua aibu na fedheha sana aise 🐒
 
Back
Top Bottom