Tusikwame kwenye udaku pekee

Tusikwame kwenye udaku pekee

KAYGREKO

Member
Joined
Jan 18, 2013
Posts
37
Reaction score
32
SI UDAKU PEKEE…
Mbali ya sifa ya kupenda habari za udaku ambazo huwafanya wabongo wengi kukesha mitandaoni, kuna upande wa pili wa wabongo ambao wanayoyajadili mtandaoni hayana kabisa uhusiano na wale wa kundi la udaku. UTASUUZIKA NA MOYO YAKO UKIWASIKILIZA. Na hasa kama huna ile hulka hasi ya kupinga na kuponda kila kizuri kinachofanywa na wengine.

Nami nilipokatisha kusoma habari za Sabaya kufungwa miaka 30,nikaamua kuperuzi na nikakuta wabongo - youtube - wakijadili TUZO YA ABDULRAZAK GURNAH INATUFUNDISHA NINI TANZANIA.?
Nikawa najiuliza hivi kweli wale wa kundi la kwanza hata wanamjua huyo Abdulrazak Gurnah?
Nikajikuta nimeganda hadi mwisho.( Nasikitika sikukiwahi live)
Kumbe kuna waTZ wenzetu wana mengi mazuri ambayo kwa bahati mbaya hatupati nafasi ya kuyajua. Hata links tunazofowadiana ni zile tu za bongo fleva, video za hapa na pale na wala hatupati wasaa wa kujua yepi mazuri yanayofanywa na wenzetu.

Inabidi waTZ tujizoeshe kufowadiana taarifa njema za yanayofanywa na wenzetu popote walipo hata kama hatuwapendi. ANZA JAPO MARA MOJA KWA WIKI KUFOWADI TAARIFA CHANYA ZA WABONGO.ZIPO NYINGI MNO.Ondokana na ile fikra mbovu na ya kukatishana tamaa kuwa wabongo hatuwezi kubadilika. Kwani hao wengine waliobadilika wamewezaje? Of course tuna udhaifu wetu lakini hatupaswi kuendelea kubaki ktk hali hiyo.
Nahitimisha kwa kumpongeza mno mwendesha kipindi cha Kijiwe mada moto na wale waliokiandaa na wote walioshiriki. Mungu awabariki. Amen.

Kama utapata fursa, hebu wasikilize wabongo hawa

KAYU LIGOPORA
ATHENS-GREECE
17/10/2021
 
Back
Top Bottom