Autodidacts
JF-Expert Member
- Jun 9, 2021
- 1,165
- 1,804
Nimefuatilia malalamiko na mijadala mingi kuhusu ujio wa 'lugha za Mdude' kwa watawala. Tujifunze kidogo kuvaa viatu vya watu wengine ata kama havitutoshi.
Mdude ni muhanga wa utawala katili kuliko tawala zote tangu uhuru. Amepewa kesi ya kubambika kama iliyothibitika hivyo kwa maandishi ya hukumu yake kuwa polisi walimiliki funguo/nyumba ya Mdude kwa siku kadhaa na ndio hao hao wakamkagua baadae na kudai kumkuta na madawa ya kulevya.
Ni pandikizo la kijinga kabisa, na linathibitisha kuwa,ama askari wetu mbinu zao ni za kitoto na hawana exposure ya mbinu za kijasusi au walifanya makusudi kuweka upenyo ili Mdude apite baada ya hao polisi kuchoka na maagizo ya uonevu kwa raia toka kwa Mwendazake .
Ameteseka kwa muda mrefu sana kwa kosa la kusingiziwa, na muda wote hakuna uongozi wa CCM uliopinga uonevu huu.
Alipotoka,hakuna alieomba radhi kwa ukatili wa kijinga aliofanyiwa Mdude. Kapoteza heshima na kudhalilishwa. Kisaikolojia ana hasira,chuki n.k. kwa waliomtesa kwa makusudi kisa kuwa upinzani.
Rais SSH amejitambulisha kuwa hana tofauti na mwendazake aliemtesa Mdude,unataka Mdude amsifu?
Kama lugha ya Mdude haiwapendezi baadhi ya watu (maana wapo wanaona ni lugha stahiki) basi lawama ziende kwa CCM na uongozi wake waliomtengeneza Mdude.
Kama Rais SSH ni mstaarabu kama anavyonadiwa na baadhi ya wafuasi wake basi angeomba radhi kwa watanzania kwa mengi machafu yaliyotendwa na mtangulizi wake.
Kwa kujinadi kuwa yeye na mwendazake ni kitu kimoja basi akubali kubeba na matokeo ya dhambi za mwendazake bila kulalamika. Kulalamikia ulichokitengeneza mwenyewe ni ujinga.