changaule
JF-Expert Member
- Jan 10, 2020
- 6,039
- 10,151
Kuna mahali, Ihefu imeizidi Yanga hasa wanapocheza nao pale Highland estate.
Mechi ya jana ni kama marudio ya mechi ya msimu uliopita.
Tuliamini Nabi ni kocha bora, kocha mzuri sana aliyeifanya Yanga iwe unbeaten kwa michezo zaidi ya 40 lakini kaja kuumbuliwa na Ihefu na sherehe ya unbeaten ikaishia hapo.
Ukiangalia mechi ya msimu uliopita na msimu huu haijatofautiana matukio.
1) Nabi na Gamond wote walifelishwa kutokana uchaguzi wa wchezaji na bahati mbaya wote wawili wamewatumia Moloko, Mauya na Sureboy kwenye kikosi kinachoanza. Sijui ni mazingira gani yanayowasukuma kuwa kigugumizi cha kushindwa kujua mapungufu ya hao watu kwenye mechi ngumu ya away.
Gamond hakuwahi kumpa Mauya zaidi ya dakika 20 uwanjani na mara zote alikuwa ana muingiza dakika za lala salama, lakini jana anakuja kuingia mtego kwa kumuanini mchezaji ambaye haaminiki. Mbaya zaidi kawajaza wachezaji ambao waliokosa match fitness na waliokosa kujiamini kutokana na kutocheza mara kwa mara. Nadhani hata yeye akikaa kwa kutulia baada ya mechi anaweza akajikataa kama ni yeye kafanya jambo kama hilo. Lakini kwake halitakuwa wa kwanza kukosea, Nabi mbele ya sherehe za unbeaten kaumbuliwa na Ihefu na hakuna aliyeamini tena ni Nabi tuliyemuamini, Nabi tuliyemuimba, Nabi aliyebatizwa uprofesa kashindwa kusherekea sherehe ya unbeaten mbele ya Ihefu.
2) Magoli ya mapema zaidi kwa Yanga
Mechi ya msimu uliopita Yanga alipata goli la mapema kabisa dakika ya 9 tu huku mechi ya jana tena Yanga wanatangulia kupata goli la mapema kabisa dakika ya 3 tu .
3) Timu kuzidiwa na kukosa utulivu baada ya kupata goli.
Mwaka jana, Baada ya Bangala kuifungia goli, iliwaamsha Ihefu huku wachezaji wa Yanga wakianza kupoteana na kutoka mchezoni kwa kushindwa kucheza mpira wao uliozoeleka.
4) Aina ya magoli ya kusawazisha
Msimu uliopita Ihefu waliweza kusawazisha goli kupitia mpira wa kutengwa, jambo ambalo limekuja kujirudia kwenye mchezo wa jana.
5) Vurugu kutokana na kuhamaki.
Msimu uliopita benchi la ufundi la Yanga walihamaki na kusababisha rapsha za hapa na pale kama ilivyokuwa jana kwa benchi la ufundi la Yanga kulikuwa na fujo za hapa na pale na mashabiki nao wakasababisha vurugu.
Mashabiki wa mpira, mpira una mambo mengi nje na ndani ya uwanja tusiishie kunyosha vidole tu kwa Gamond lakini hatujui alikumbwa na mazingira ya namna gani kimaamuzi. Na pia tukumbuke Nabi pamoja na uprofesa wake na Mayele akiwa ndani ya uwanja walipoteza mechi. Mwisho ni kwamba uongozi wa Yanga na ufundi tutumie hii mechi kama funzo kwetu tusikosee tena kuzicheza hizi mechi hasa za mkoani japo kwa msimu uliopita tuliweza kwa asilimia kubwa hivyo tujifunze tulipokosea.