GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Ni kweli kwamba Mchezaji Mohamed Banka kutokea Zanzibar ambaye amesajiliwa na Yanga SC amehukumiwa Kifungo cha miaka miwili kwa Kosa la Kutumia dawa za Kulevya aina ya Bangi / Bange. Sitaki kumtetea na katika hili naweka pembeni Usimba wangu ( ambao kila Mtu anaujua humu ) ila ninachowaomba Wanamichezo wenzangu ni kwamba kupitia huyu Mchezaji basi tuweze pia kuwasaidia Wachezaji wengine wenye hii tabia waweze kubadilika.
Binafsi tokea niwe Mchezaji wa Mpira kwa ngazi ya Shule ya Msingi, Upili na kidogo Chuo Kikuu nimeweza kushuhudia Wachezaji wenzangu wengi tu wakiwa wanavuta Bangi tena tukiwa Kambini kabisa. Hivyo tatizo hili ni la Mzizi mrefu na Jamii ya Wanamichezo inatakiwa ishirikiane ili kulimaliza kama siyo kulikabili.
Kwa Tasnia yangu na tabia yangu ya Kupenda Kujichanganya sana na Watu wa kila Kada na Kila rika nisifiche hapa nina Wachezaji tena ' Waandamizi ' kabisa wa Vilabu vya Simba, Yanga, Mtibwa Sugar na Azam FC ambao kwa bahati nzuri ni Marafiki zangu wazuri tu na wakubwa lakini nadhani kama kuna siku ambayo watakuja kuacha Kuvuta Bangi / Bange basi labda ni pale tu Wakifa kama siyo Kufariki.
Sema tu ni bahati mbaya sana hili ' Zigo la Lawama ' limemwangukia huyu Mchezaji mdogo wangu Mohamed Banka lakini Kaka zake wengi ( namaanisha Wachezaji Waandamizi ) wanavuta mno Bangi / Bange. Kuna Mchezaji mmoja ( namuhifadhi ) alikuwa anachezea Klabu yangu ya Simba anaishi Kimara hata muda huu ukienda Nyumbani Kwake utawakuta Wachezaji wengi Waandamizi wakiwa wanavuta nae Bange / Bangi.
Kuna Mchezaji mwingine nae ni Rafiki yangu mzuri tu anachezea Yanga SC huyu Yeye iwe ni Mazoezini au katika Mechi asipoletewa Bangi / Bange na Viongozi wake anaweza hata akasusa Kucheza hivyo Klabu huweka kabisa Bajeti yake ya Kumnunulia hicho Kilevi na huwa hachezi bila kuonyeshwa ama Kadi ya Njano au Nyekundu a.k.a Umeme.
Kuna Mchezaji mmoja tena Mwandamizi kabisa wa Simba SC ambaye ' Maskani ' yake kubwa ni Kawe karibu na Baa maarufu ya Maasai ana Urafiki na Mchezaji mmoja Mwandamizi wa Mtibwa Sugar ambaye Kaka yake alipigwa Risasi njia panda ya Kawe na Mtawala mmoja ambaye nae alikufa baadae. Huyu Mchezaji wa Simba SC Bange / Bangi zake zote anazipatia hapo hapo Kijiwe chao cha Kawe na ndiyo amemuharibu sasa na Mchezaji mwenzake mgeni ambaye alianza Kukubalika mno katika nafasi ya Beki wa Kati lakini baada ya ' Kuonjeshwa ' tu hicho Kilevi sasa hata Kiwango chake Kimeshuka.
Nina mifano mingi na hunidanganyi kitu kuhusu Wachezaji wa Tanzania na matumizi yao ya Bangi / Bange na hapa wala hawa Viongozi wa hivi Vilabu wasiwadanganye kuwa hawajui kwani wao ndiyo huwaagizia na wapo pia hadi Viongozi na Makocha wa hivyo Vilabu nao ni Wadau / Watumiaji wazuri tu wa Bange / Bangi.
Namalizia tu kwa kusema tuache Kumsakama huyu Mchezaji Mohamed Banka kwakuwa tu ameonekana Yeye bali tumsaidie Kisaikolojia ili aweze Kubadilika kusudi basi na Wachezaji wengine kupitia Yeye waweze Kubadilika na hatimaye kulitatua hili tatizo. Na kinachoniuma na kunikera ni kwamba kuna hadi Watangazaji na Waandishi wa Habari za Michezo nchini ambao ' personally ' kabisa nawajua kuwa ni Wavutaji wazuri wa hiyo hiyo Bange / Bangi lakini na wao leo hii wanajifanya ' Kumshambulia ' huyu Kijana wa Watu kana kwamba Yeye ndiyo mkosaji pekee wa hili Sakata.
Nawasilisha.