LGE2024 Tusio na ajira/kazi zenye kuingiza kipato haturuhusiwi kugombea nafasi yoyote ya kisiasa

LGE2024 Tusio na ajira/kazi zenye kuingiza kipato haturuhusiwi kugombea nafasi yoyote ya kisiasa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Wakusoma 12

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2017
Posts
4,035
Reaction score
11,462
Wakuu nafikiri wote tumesikia kuwa wagombea kadhaa wameenguliwa kugombea nafasi mbali mbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kile kinachodaiwa kutokuwa na shughuli za kuwaingizia kipato yaani kazi. Sasa vijana wenzangu wasomi ambao hatuna ajira ila tu tumeamua kufanya siasa serikali ya CCM haitaki.

Tupeane maoni tunafanyaje wakuu? Nchi hii mambo mengi yanapelekwa kihuni. Moja kati ya sifa ya kugombea cheo cha siasa ni kwamba usiwe mtumishi wa Umma, Sasa swali tunalouliza hao madogo chipukizi wa CCM viongozi wao wanafanya kazi Gani na wapi?

Je, hao wagombea wanaoenguliwa Huwa wanapatiwa ruzuku na serikali ya kuendeshea maisha yao? Imekuwaje serikali ikadai hawana kabisa shughuli?
 
Wakuu nafikiri wote tumesikia kuwa wagombea kadhaa wameenguliwa kugombea nafasi mbali mbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kile kinachodaiwa kutokuwa na shughuli za kuwaingizia kipato yaani kazi. Sasa vijana wenzangu wasomi ambao hatuna ajira ila tu tumeamua kufanya siasa serikali ya CCM haitaki. Tupeane maoni tunafanyaje wakuu? Nchi hii mambo mengi yanapelekwa kihuni. Moja kati ya sifa ya kugombea cheo Cha siasa ni kwamba usiwe mtumishi wa Umma, Sasa swali tunalouliza hao madogo chipukizi wa CCM viongozi wao wanafanya kazi Gani na wapi?
acha uvivu zidisha juhudi katika kufanya kazi halali ya uhakika na mengine utazitishiwa :pulpTRAVOLTA:
 
Ni uhuni tu wa CCM sababu wamejua wakifuata sheria na kanuni za uchaguzi hawatoboi,
mbona hao ma jobless wa CCM wote wamepitishwa nchi nzima.

Ni aibu kwa Taifa letu kama hata kujisimamia huu uchaguzi mdogo tu hatuwezi.
 
Unakuta pale kwenye eneo la shughuli yako...ukijaza Mjasiriamali watakuandikia "umeenguliwa sababu hauna kazi ya kukuwezesha kuishi"
Hawa na CCM yao wamejaza Ujasiriamali wa kuuza vitumbua.
Sasa hii tafsiri ni CCM na Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wamejiwekea.
 
Back
Top Bottom