Tusio na uwezo wakununua magari mapya tukutane hapa!

Tusio na uwezo wakununua magari mapya tukutane hapa!

KakaKiiza

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2010
Posts
11,794
Reaction score
9,075
Najua tunapenda magari mazuri na mapya ila hatuna uwezo wakuyanunua hayo magari mapya! Brand New tuna uwezo wa kununua tunaishia Befoward,SBT,etc "SECOND HAND" Tujadili hapa je uliponunua ulikuta lina matatizo gani??na je ulifanyeje kutatua tatizo hilo??karibu tuelimishane.
 
Kama unamiliki 2nd hand una afadhali, wengi wanamiliki 4th and 5th hand.
 
Nilikua sina uwezo wa kununua jipya nikaenda zangu zenji kununua sekandi hendi balaa nililokutana nalo baada ya kununua ni heri ningenunua jipyaa toka japani mana gharama ilizidi ya kuagiza jipya.
 
Nilikua sina uwezo wa kununua jipya nikaenda zangu zenji kununua sekandi hendi balaa nililokutana nalo baada ya kununua ni heri ningenunua jipyaa toka japani mana gharama ilizidi ya kuagiza jipya.

Hukutafuta fundi wa kulikagua Boss, ukamuamini muuzaji??
 
Mimi nina experience na Subaru Legacy Wagon ndio nimekuwa nikitumia na kuuza pale anapohitaji mtu, sasa haya magari naagiza beforward, kwa miaka 6 sasa naagiza kila mwaka nabadilisha maana wanao yapenda wengi, mfano nikitoka Dar kwenda Mwanza kwa siku yakwanza kulitoa bandarini linachemsha nikiwa njiani, nikagundua lina sensor iyo sensor huwa inahisi joto la engine basi nguvu ya gari na yenyewe inapungua, cha kufanya na disconect sensor naendelea na safari hadi nafika matengenezo mengine yanafuata. seat za dereva mkono wa kulia kwa chini unakuta pamechanwa kidogo kama ka mfuko sasa sijui huwa yanatumika kusafirishia vitu gani maana kila nikinunua lazima nakuta hivyo ila nampa fundi cherehani kazi ya kushona na sindano. kuna motor flan mkono wa kulia kama unafungua bonet unakuta inalika hadi sasa sijaelewa kabisa ila ndio matatizo hayo, ila ni magari mazuri yenye nguvu.
 
Ngoja nione wamiliki wa magari humu JF niliwahi kusikia JF karibia kila mtu ana gari
Mimi sina mkuu,wala cjawahi kuwa nalo huko nyuma,pia sina matarajio Kwa miaka ya hv karibuni kumiliki na hivi vyuma vilivyokaza ndio matumaini yanazidi kufifia mkuu.
 
Back
Top Bottom