Tusione aibu kuiga katiba ya Kenya kwenye mwelekeo wa Katiba Mpya

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Watanzania tunachotaka ni katiba mpya kusaidia nchi. Katiba hii mpya ambayo majadiliano yameanza sio ya vyama vya siasa ni ya Tanzania nzima kwa ujumla. Tusiwe wazito kuchukuwa na kuiga wenzetu wa Kenya kwenye vifungu ambavyo tunajua kabisa vinafanya kazi vizuri. Vifungu hivi ni pamoja

1. Tume huru na sheria zake tumeshaona Tume ya uchaguzi wa Kenya ilivyo huru
2. Uhuru wa Mahakama. Kwasasa sheria zetu za mahakama bado ni za kikoloni zibaddilike ili mahakama iwe huru zaidi.
3. Nguvu ya Bunge na Raisi. Mfano watendaji wakuu kupitia bungeni kuthibitisha ni jambo jema.
4. Makatibu wakuu ndiyo wawe mawaziri na sio wabunge. Mfumo wetu wa sasa hivi unasababisha tuwe na siasa kuliko utendaji kwenye shughuli za maendeleo. Raisi tumpe uhuru zaidi kwenye hili kumchagua mtu yeyote anayefaa. Mfumo wa sasa wa wabunge kumi hauna tija waziri ambaye kachaguliwa kwa vitu kumi vya Rais anaweza kutenguliwa lakini bado akawa mbunge! wakati Raisi alimweka makusudi ili ampe uwaziri!. Kwasababu ya mfumo mbaya wanaishiwa kupelekwa ubalozini au kupangiwa kazi nyingine ili tu kiti kiwe wazi.

Kwa ujumla sio Kenya tu lakini tuangalie na katiba nyingine
 
Wewe kweli damu ya Kenya ipo mishipani mwako.

Hiyo katiba ya kenya si ni ya Marekani, kwa nini usihimize tuige ya huko?
 
Tumehuru ya Kenya umeona ilivyopasuka 3-4 kumbe 4 wanatumiwa na deepstate muungano wa Rais na Mkuu wa ipinzani ("handshake") dhidi ya makamo wa Rais. Umeona ilvyofadhiliwa navkina Tuju na Raila, yaani washindwa? Mahakama yetu ni huru kuliko ya Kenya mara 100. Kenya hufuata kabila lako sisi hufuata sheria. Sasa deepstate imeibua whistleblower Mkikuyu wa Gatundu siyo wa Nyeri *sawa na Msukuma wa Shinyanga na Msukuma wa Mwanza, sisi hayo hatuna). Sasa ngoja waanze kuchimjana tena. Waziri lazima atokane na wabunge, awe mchaguliwa ili baadaye awaongoze watu. Ya Kenya eti Katibu Mkuu haifai kwa vile KM si mwanasiasa; ni technocrat. Kenya hakuna cha kuchukua, wao ndiyo waje kwetu.
 
Toa ushahidi kwanini mahakama yetu ya mfumo wa kikoloni ni bora kuliko ya kenya. Tanzania ukifungua kesi ya kupinga uchaguzi inachukuwa mpaka miaka 4 kwa mahakama kutoa maamuzi. Kesi Tanzania zinachukuwa mpaka miaka 5 tena kesi ndogo ndogo tu. Watu wanabambikwa kesi ya jinai na kukaa jela kwa miezi na miaka halafu waliowaweka ndani hawana cha kujibu, watu hawalipwi fidia yeyote wala nini!.. Hakuna ushahidi wowote wa maana wa kuonyesha mahakama yetu ina uhuru kuliko kenya. Hata kikwete alikubali hilo alivyoenda kenya kama muangalizi.
 
Wewe kweli damu ya Kenya ipo mishipani mwako.

Hiyo katiba ya kenya si ni ya Marekani, kwa nini usihimize tuige ya huko?

ladboy umeanza kuongelea watu badala ya hoja
 
'ladboy', ndiyo kitu gani?

Huoni nimeongelea katiba au hujui kusoma na kuelewa?
Hawa wanaogawa uraia kama njugu ni wahujumu wakubwa wa nchi.
 
Tumehuru ya Kenya umeona ilivyopasuka 3-4 kumbe 4 wanatumiwa na deepstate muungano wa Rais na Mkuu wa ipinzani ("handshake") dhidi ya makamo wa Rais. Umeona ilvyofadhiliwa navkina Tuju na Raila, yaani washindwa? Mahakama yetu ni huru kuliko ya Kenya mara 100. Kenya hufuata kabila lako sisi hufuata sheria. Sasa deepstate imeibua whistleblower Mkikuyu wa Gatundu siyo wa Nyeri *sawa na Msukuma wa Shinyanga na Msukuma wa Mwanza, sisi hayo hatuna). Sasa ngoja waanze kuchimjana tena. Waziri lazima atokane na wabunge, awe mchaguliwa ili baadaye awaongoze watu. Ya Kenya eti Katibu Mkuu haifai kwa vile KM si mwanasiasa; ni technocrat. Kenya hakuna cha kuchukua, wao ndiyo waje kwetu.
Uongo mtupu,
 
Back
Top Bottom