Mtoto wa Jadu
JF-Expert Member
- Jun 26, 2018
- 419
- 1,020
Tukiachana na muziki, burudani inayofuatiwa kwa kupendwa na wengi ni mpira!
Lakini imekuwa bahati mbaya kwa mpira wa hapa nyumbani, umebebwa na timu mbili tu za Simba na Yanga.
Hali imekuwa mbaya sana katika ushabiki wa timu hizi, umevuka mipaka, umeingia mpaka sehemu rasmi kabisa kama vile kwenye majumba ya ibada, na hata siasani huko bungeni. Watu ni kuzungumzia simba na yanga tu
Ni mara kadhaa sasa nimeashuhudia, ushabiki wa simba na yanga ukihusishwa katika maeneo kadhaa.
Sikuhizi, aghalabu kwenye sendoff na sherehe kama hizo, unakuta watu wanaleta zawadi zao katika mtindo wa usimba na uyanga!!
Jambo hilo sio wote tunalifurahia!!
Sasa, inapotokea mechi baina ya hizo timu, stori mitaani inakuwa ni hiyohiyo, nothing else!!
Kibaya zaidi, timu hizo zinapambwa na maneno mengi sana kuliko uhalisia... Yaani mashabiki wao wamekuwa waongeaji sana, kutetea timu zao, ilhali hata hazitufaidishi na chochote kama taifa.
Hakuna maendeleo kisoka tunayoyapiga kutokana na simba na yanga, japo ukiwasikiliza wenye timu, wanaweza hata wakakumeza [emoji28]
Karibuni muongezee.. [emoji116]