Tusiotaka Katiba Mpya tukutane hapa

Tusiotaka Katiba Mpya tukutane hapa

ong'wafaza

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2012
Posts
247
Reaction score
107
Binafsi nimekuwa nikifuatilia mijadala ya vuguvugu la madai ya Katiba Mpya sambamba na kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na pande mbili zinazosigana kuhusiana na swala hili la Katiba Mpya.

Hebu kwanza kabla hatujaingia kwa undani kuhusu hoja ya sisi tusiotaka na wanaotaka katiba mpya tujiulize yafuatayo:

1. Je, ni kweli uhitaji wa katiba mpya ni mhimu kwa sasa?
Na kama ni mhimu, umuhimu wake ni upi?
Na kama sio mhimu ni kwa nini baadhi ya Wananchi wanataka katiba mpya?

2. Wanaotaka katiba mpya wanaidai au wanaiomba?
Tukumbuke kuwa, kudai na kuomba kitu ni mambo mawili tofauti sana.
Anayeomba anaweza akapewa au akanyimwa kwa kuwa anayaombwa anakuwa na hiari ya kutoa au kutotoa anachoombwa.
Lakini madai huwa yanaambatana na msukumo au presha fulani kwa anayedaiwa, na presha ikizidi huwa inafika mahala mdaiwa analazimika kutoa,atake asitake.

3. Wanaotaka katiba mpya idadi yao inaongezeka au inapungua?
Kama inaongezeka, je ni kwa kiasi gani?
Tukumbuke kuwa kuongezeka au kupungua kwa idadi kunashabihiana moja kwa moja na kuongeze au kupungua kwa presha ya madai.

4. Je, endapo Katiba inayotakiwa itapatikana kwa presha ya wanaoitaka,italeta madhara gani kwa Taifa?
Baada kupta majibu ya hayo maswala manne hapo juu, sisi tusiotaka katiba mpya tunaweza kuamua, na kwa kutanguliza uzalendo mbele, kama tuendelee namsimamo wetu au la.

Binafsi nisingependa kuona Katiba Mpya inapatikana kwa presha ya wanaotaka Katiba Mpya.

Lakini pia nisingependa kuona Taifa letu likipuuza wanaodai Katiba Mpya hata kama ni wachache kwa sasa na kusubiri mpaka wawe wengi.

Presha ya wengi ina madhara makubwa kwa Taifa letu.

Tutangulize uzalendo kwenye kufikia uamzi sahihi na si kutanguliza maslahi binafsi au maslahi ya kukundi fulani.

Mungu ibariki Tanzania, na KAZI IENDELEE.
 
Sijaona hoja yoyote umeweka kukataa Katiba Mpya

CCM hawataki katiba mpya maana wanaona itaweka rehani maslahi Yao, itapunguza nguvu ya Rais kuingilia mihimili mingine, itawaweka kando na wizi wa kura maana ndani yake Tume huru ya uchaguzi itakuwepo

Katiba mpya muhimu sanaaa ili kusaidia kusimamia nchi yetu hasa kuhusu uwakibikaji, ufanisi kazini, kuondoa viongozi mzigo, kuwajibisha wabunge wajinga wajinga, kuwashighulikia kikamilifu mafisadi, kupunguza gharama za kuendesha nchi

Katiba mpya muhimu Sana Tena sana
 
Back
Top Bottom