Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
RAIS ASIZUNGUKWE NA WATU WENYE UKABILA NA UDINI.
Na, Robert Heriel
Tupo katika kipindi cha Kampeni, leo ndio ufunguzi wa Kampeni za Uchaguzi. Huu ni wakati muhimu kwa taifa letu.
Tunachagua viongozi watakaotuongoza kwa miaka mitano.
Tunapaswa tuchague viongozi wasio na dalili za ubaguzi wa kidini, ukabila ama ubaguzi wa aina yoyote ile.
Tunapaswa kuchagua viongozi ambao hawajawahi kujiingiza katika kauli za kibaguzi, iwe kidini au kikabila.
Bila kujali chama, nafasi ya mtu, ikiwa mtu yeyote kutoka Chama chochote aliwahi kuhusika na kauli za kibaguzi, asichaguliwe. Huyo hatufai, ni mtu wa hovyo.
Ukisikia ubaguzi unatokea katika nchi, basi jua wanaomzunguka Rais ni wabaguzi. Kama wanaomzunguka Rais sio wabaguzi, sio rahisi kwa Rais kupata nguvu ya kubagua watu.
Mtu yeyote mwenye shutuma za Ukabila, iwe kwa kuhamasisha, kutoa kauli au namna yoyote ile hapaswi kuchaguliwa. Hili nitalisema leo, kesho na hata milele.
Kuendekeza watu wabaguzi ni kuweka amani ya nchi rehani.
Mifano ya watu waliogombea na wanashutuma za Ubaguzi iwe wa Kikabila au kidini, na vithibitisho vipo, ni Pamoja na Askofu Gwajima.
Askofu Gwajima na watu wenye tabia kama zake, wasichaguliwe bila kujali wapo chama gani.
Gwajima asichaguliwe
Gwajima asipewe kura
Gwajima hafai kuwa karibu na Rais.
Endapo watu kama Gwajima wenye kuhusishwa na ubaguzi na shutuma za ubaguzi wakimzunguka Mhe. Rais, nakuhakuhakikishia ubaguzi utakolea nchi hii.
Wabaguzi wasichaguliwe
Wadini wasichaguliwe
Wakabila wasipewe kura.
Jambo hili sio suala binafsi, bali ni suala linalohusu maslahi ya taifa.
Uwe ni CCM
Uwe CHADEMA
Uwe ACT- WAZALENDO
Kama unatabia za ubaguzi hatutakupa kura.
Nimemtolea mfano Gwajima kwa sababu ndiye mtu ambaye nimeshawahi kumsikia mara kwa mara akihusishwa na mambo ya ubaguzi wa kidini,na kikabila.
Gwajima usije ukahisi ninakukandia usiwe Mbunge, hapana, bali sitaki watu wenye tabia kama zako wamkaribie Rais, ama waingie kwenye nafasi za juu za kufanyia maamuzi ya nchi hii.
Ninashida na kauli zako, wewe na watu kama wewe.
Hata hivyo muda wa kuomba msamaha si sasa.
Muhimu: Mbaguzi yeyote asipewe kura. Kumpa Kura mbaguzi ni kuupa nguvu ubaguzi, ni kuunga mkono ubaguzi
Najua kila mmoja anahistoria yake na anajua ubaya wa ubaguzi.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300