Tusipobadili mitaala mapema hali itakua mbaya zaidi

Tusipobadili mitaala mapema hali itakua mbaya zaidi

Libadi

Senior Member
Joined
Apr 13, 2018
Posts
142
Reaction score
198
Habari za mchana wakuu Kuna kitu Kwa upande wangu nashindwa kukielewa.

Kuna tatizo kubwa la ajira nchini nimejaribu kufatilia hatua mbali mbali ambozo Taifa linachukua Bado sioni kama zinaridhisha. Swali langu kwanini selikali isibadili mitaala?

Kuna gharama Gani kuibadili mitaala iliyopo inazalisha watu wengi wa kukaa maofisini.

Leo hii Fanya tafiti mdgo tu. Nenda shule za msingi uliza watoto unataka kuwa nani badae watakujibu doctor,Mwalimu,nesi n.k

Hizo kada tayari zimejaa na waliopo benchi ni wengi mnoo. Ni muda wa selikali kubadili mitaala ambayo itaendana na Dunia ya Sasa.

Moja ya njia ya kupunguza tatizo la ajira ni kubadili mitaala toka chini Hadi juu. Elimu ya Sasa haiwezi kuondoa tatizo la ajira zaidi inaongeza tatizo.
 
Mitaala peke yake kubadilishwa haitatosha. Mazingira na miundombinu pia, Viwanda vidogo dogo vimekewa mazingira Gani? Fani za kilimo na uzalishaji vimekewa mazingira Gani?
 
Mitaala peke yake kubadilishwa haitatosha. Mazingira na miundombinu pia, Viwanda vidogo dogo vimekewa mazingira Gani? Fani za kilimo na uzalishaji vimekewa mazingira Gani?
Umemjibu vizuri kabisa. Ningependa suala lisiwe mitaala kwani hata hiyo mitaala mipya itakutana na miundo mbinu na beaurocratic and difranturized system ile ile kwa hiyo matunda yatakuwa yeleyale.

Ifanyike a thorough situation analysis ya elimu yetu toka primary mpaka university na ifanywe na wataalamu independent wenye exposure ya education system nchi mbalimbali na zilizofanikiwa. Watoke na ushauri uliotailored na setting zetu na serikali iwe tayari kuuimplement.
 
Kikwazo kikubwa ni lugha.tumenywimwa fursa nyingi sababu ya kiswahili chetu ambacho hakina tija Kwa Dunia ya Sasa.Ilifaa kiswahili tuzitumie kama tungekuwa na uwezo angalau 70%ya mahitaji yetu tunajitengenezea wenyewe.Wanaotuhamasisha tujifunze kiswahili,watoto wao wanasoma international ambako kiingereza ni lazima
 
Nimeomba kazi kwenye chuo nilichosoma wanasema hio kozi haitambuliki wakati wamenifundisha wenyewe
 
Back
Top Bottom