Tusipochukua maamuzi magumu Taifa letu la Tanganyika litapotea kabisa

Hapa nimekuelewa sana mkuu tena sana...
 
Mpaka sasa kwa sheria za Tanzania, hakuna Afisa Usalama anaweza kushitakiwa kwa muaji makubwa yaliyofanyika Tanganyika na yanayoendelea kufanyika, hii ni kutokana na Kifungu cha 23 cha sheria ya TISS 2023. Wamepewa kinga (Immunity from Prosecution). Haya mabadiliko hayakuwa ya bahati mbaya. ​
 
Kwa hio wa kushtakiwa ni .........?
 
NDUGU WATANGANYIKA mnaanza kuelewa somo au bado mnaendelea kukomaa ???​
 
WATANGANYIKA hivi hata mlielewa nilichokiandika kuhusu hii sheria ya TISS ???

MNATACHELEWA MNOOOO!
​
 
Ukiwa serious basi umuombe Mungu abadilishe hali yenyewe ikishindikana basi sisi hakuna chakufanya maana wameshajiamulia mambo yao
 
Hili ni gumu sana kulimeza, lakini kiuhalisia ni vigumu sana mtu kuwa mwanaharakati au mwanamapinduzi akishavuka miaka 25. Ukiona mtu kaanza harakati ameshakuwa mtu mzima kabisa, basi fahamu fika aidha ni Pandikizi, Kibarua au Kapoteza mwelekeo wa maisha.

Uzoefu wa kihistoria, unaonyesha kwamba wanamapinduzi wengi duniani kote huanza harakati kipindi cha ukuaji na ukomaaji wa tabia (Formative Years), ambapo huanzia miaka 13-25. Hiki kipindi ndicho ambacho tabia ya kijana na falsafa yake nzima ya kimaisha hujengeka. Mtazamo mzima wa kidunia na jinsi anataka iweje huonekana kipindi hiki. Kubwa zaidi kipindi hiki, mtu huwa ni rahisi mno kufundishika na kupokea mawazo mapya.

Ndiyo maana hata taasisi nyingi za kiusalama, kiflateli na zile za kidini, hutafuta vijana kuanzia miaka 14-25, wakiamini kwamba ni rahisi kuwafundisha (Easy to train) na kuwapandikiza mawazo mapya (Easy to indoctrinate). Ubongo unakuwa hauna mambo mengi na wanakuwa hawana majukumu, hivyo hawana mengi ya kupoteza.

SASA BASI: Ukiona katika kipindi hiki, ghafla tu katokea Nabii Mzee au Mwanaharakati Tajiri mwenye mengi ya kupoteza, fungua macho yako kwa ukubwa. Ukweli ni kwamba historia huwa haiwatendei haki WANAHARAKATI HALISI:

Mosi, wanaharakati na wanamapinduzi wote hujengwa kwenye msingi wa falsafa fulani. Asilimia zaidi ya 90% mengi ambayo mwanaharakati au mwanamapinduzi huyasimamia akiwa na miaka 50 huanza kuyaamini akiwa na miaka 14-25. Nadra sana mtu wa miaka 30 akaanza kuwa mwanaharakati au mwanamapinduzi. Wote unaowaona hapa nchini, kama Lissu, Warioba, Nyerere, Kambona, Babu n.k walianza kuwa na imani zao wakiwa wadogo mnooo.

Pili, wanaharakati na wanamapinduzi wote huishi maisha ya kupunjwa na dunia. Huwa hawapati raha ambazo watu wengine tunazipata. HII NI KATI YA SIFA KUU. Mara zote huwa hawana mali, na hawavutiwi na utajiri ambao wengine tunautumikia. Ukiona mwanaharakati anafanya biashara na tajiri mkubwa, fungua macho kwa ukubwa na kuwa makini. BWANA YESU alisema "Huwezi kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja, aidha utamdharau huyu na kumpenda huyu" akaendelea kusema "Huwezi kutumikia fedha na MUNGU"

Mara nyingine hata maisha ya familia huwa hawana. Anaweza akawa na mke na watoto ila akalazimika kuwa nao mbali. Mara nyingi hata familia zao huwa haziwaelewi kwasababu wamejitoa kutumikia falsafa zao, jambo ambalo huwazuia kuwa wazazi wazuri.

=========================================
Kiufupi MWANAMAPINDUZI au MWANAHARAKATI huwa hawezi kupata vyote ambavyo dunia inatoa. Ni lazima akubali kubeba msalaba wake na kutoa sadaka baadhi ya vitu anavyovipenda.

Hapa nchini Tanganyika, tumepelekeshwa na upepo kwasababu tunaamini watu kwa haraka. CHADEMA kwa miaka mingi waliamini MWAMBA ni chuma, lakini ukweli ulikuja kufahamika kwamba alizipenda harakati na mapinduzi, lakini hakuwa mwanaharakati. Hakuweza kulipia ile gharama.
======================================================

Kiufupi, HAKUNA MWANAHARAKATI ambaye hajalipia gharama kubwa kwenye maisha.
Ukiona mtu anasema yeye ni MWANAHARAKATI basi chunguza maisha yake sana. Ukiona mwili wake umejaa majeraha, basi huyo mwamini kwa maisha yako yote, ila laaah, kimbia.


ENIWEI, hili nalo ni gumu kueleweka.....
​
 
Bado mnakomaa tu,

Wabongo mpaka muone damu na moshi wa bunduki ndiyo akili zitawakaa vizuri!
​
 
Bado mnakomaa tu,

Wabongo mpaka muone damu na moshi wa bunduki ndiyo akili zitawakaa vizuri!
​
Kwamba watu waache agenda waanze kudili na personalities kwa majina ya kubatiza, kuwa Mwanaharakati, huyu Mwanasiasa na huyu msaliti?

Vifikra finyu fulani, vya unataka mwenda Kivukoni, badala kuangalia njia ya kukufokisha wewe unakaza fubu la majina ya isafiri kama bajaj, Daladala, Guta, Mwendokasi??

Vi-mindset fulani vya mwaka 1778
 
Nimesoma thread nikidhani ni mpya ila kila nikipitia neno naona lipo familiar. Kumbe nimeshausoma

Ni thread makini πŸ™πŸ½πŸ™πŸ½
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…