Tusipochukua maamuzi magumu Taifa letu la Tanganyika litapotea kabisa

Mabadiliko hayawezekani bila maumivu ya kutosha. Watanzania kwa ujumla wameridhika na maisha yao chini ya viongozi wote tangu tupate uhuru. Mamilioni wangekuwa wanaumia sana, kungekuwa na maandamano nchi nzima, kila wilaya, kila mkoa, kila wiki hata isingekuwa kila siku. Hakuna askari wa kutosha kuwazuia. Hata jeshi lisingeweza kuwazuia.

Kitu ambacho Watanzania muombe kisitokee ni jeshi kuingilia na kuchukua madaraka. Mtajuta. Watavuruga nchi, kutakuwa na umwagaji wa damu na hakuna yeryote atakayewazuia. Wasemacho ni sheria. Bishana nao, angalia mtutu wa bunduki. Mapinduzi yaliyotokea nchi mbalimbali za Kiafrika hayakutatua matatizzo, licha ya kuleta vurugu nchini pamoja na umwagaji wa damu. Tumefanikiwa kufanya mabadiliko makubwa nchini bila kumwaga damu tangu enzi ya Mwalimu Nyerere. Ujamaa uko wapi sasa? Tulimwaga damu? Damu ilyomwagika 29 October na baada ya hapo yalileta mabadiliko gani ya manufaa kwa taifa? Maisha yaliyopotezwa yamesaidia nini kuleta mabadiliko nchini? Damu ikimwagika tena, maisha ya mamia na maelfu yakipotea tena yatalisaidia taifa?

Haraka haraka haina baraka. Kuna uwezekano mkubwa sana hakutakuwa na mabadiliko yoyote mwaka 2030. Vumilia. Epukana na vurugu na umwagaji wa damu. Mabadiliko yanakuja. Tegemea kuwa na mabadiliko makubwa kuanzia 2035. Tukifika salama, tutakuwa na Tanzania tofauti kabisa na ambayo tuliyonayo sasa mwaka 2040. Mvumilivu hula mbivu. Siaimini hata kidogo Tanzania ya leo itakuwa hivyo 2040.
 
Kwa hali hii tuliyo nayo bora Jeshi lichukue maana hakuna chochote cha faida.Si siasa,uchaguzi,demokrasia,mfumo wa uendeshaji nchi,uchumi na utamaduni wa Mtanzania vinavyozingatiwa.
 
Baada ya mwaka tangu hii post ninaiona Tanganyika imezama na matuamini ya kuibuka ni baada ya miaka 10 mbele ni giza totoro lililosababishwa na familia chache tu na waliokuwa na jukumu la kuzuia hili wamewekwa mateka na familia hizi za majambazi, mafisadi na wala rushwa.
 

Uhuru wa mahakama upo mashakani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…