Nikupateje
JF-Expert Member
- Dec 22, 2009
- 1,334
- 989
Inaelekea draft ya katiba imetupotosha na kusahau jambo la msingi kuliko yote. Moja ya mambo ambayo yalifanya vyama vya upinzani kutaka kugomea process ya katiba mpya ni kubadilishwa kwa sheria inayotaja compsition ya wajumbe wa bunge la katiba au Bunge Maalum.
Tunafahamu kwamba Bunge lilijitungia Sheria hii na kujichagua lenyewe liwe mjumbe wa Bunge la Katiba yaani wabunge wote wa sasa na wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wawe wajumbe wa bunge hili.
Kwa maana hiyo Bunge la Katiba litakuwa na zaidi ya asilimia 66 (absolute majority) ya wabunge wa CCM na hivyo itakuwa katiba ya CCM.
Tunavyojua wabunge wa Bunge la Jamhuri hawakuchaguliwa ili kutunga katiba bali walichaguliw ili kutunga sheria za kawaida.
Hoja hii haikuweza kupingika na hata Waziri Mkuu mwanzoni mwa kikao hiki cha bajeti March 2013, alisihi vyama hasa Chadema kisijitoe bali sheria ya marekebisho italetwa bungeni kabla ya kuisha kikao hiki cha Bajeti ili tujue ni akina nani wataingia kwenye bunge la katiba.
Hivyo, Chadema na vyama havikujitoa vikaahidi kusubiri kuisha kwa bunge hili la bajeti ili tuone serikali italeta vipi huo muswada wa kurekebisha watakaoingia kwenye Bunge Maalum la Katiba.
Sasa bajeti ya serikali imepitishwa. Kilichobaki na kinachoendelea sasa ni miswada ya kadhaa.
Kwa kelele zote zile za mwanzo nilitegemea sasa hivi kila mmoja wetu apige kelele kuwa sasa ni wakati muafaka wa kuona ni vipi serikali inapeleka muswada kurekebisha composition ya bunge la katiba ili kusiwe na kundi lenye majority na eventually likawa kama ndiyo decison maker inapofika kupiga kura.
Inaeleka kila mmoja hata wasomi wanaolielewa jambo hili kana kwamba kutolewa kwa rasimu ya katiba kumewafumba macho hadi wasiweze kuona jambo hili.
Hata Kitila Mkumbo nimeona maoni yake kwenye gazeti moja akilalamika kwamba wingi wa CCM kwenye bunge la Katiba unaweza kuwa kiwazo ikawa katiba ya CCM na si ya wananchi.
Kauli kama hizi ni za kukata tamaa maana ni kama vile mahesabu yalipigwa kwamba ikitoka rasimu basi kila mmoja atajikita kwenye rasimu na tutasahau kudai sheria ya kubadili wingi wa wabunge kwenye bunge la katiba.
Kama ni mahesabu yalipigwa basi inaelekea yanafaulu maana hakuna sasa anayechangamkia hii topic ya Bunge la katiba na hivyo wanaofaidika na kuzubaa kwetu wanachekelea na wanaweza kuudhika na thread kama hii kwa sababu ninakumbusha kisichotakiwa kukumbushwa kwani ukimuamsha aliyelala utalala wewe.
Kikubwa ni kwamba Waziri Mkuu kwa mdomo wake bungeni aliahidi kuleta muswada kama nilivyosema. Sasa, haina maana kupiga kelele kuhusu uzuri au ubovu wa rasimu wakati tunaacha kupiga kelele kuhusu mabadiliko ya sheria wakati rasimu hata ikiwa nzuri vipi, wakijazana wabunge mle kwenye Bunge la Katiba wote tunajua yatafanyika yaleyale ambayo hufanyika Dodoma.
Wataulizana kifungu hiki cha kutokuwa na Serikali ya Tanganyika kinaafikiwa? Watajibu Ndiyooooooooooooooooo. Sasa usiyetaka utafanya nini
Mwisho katiba ikikaa kama wanavyotaka wao wataulizwa na Spika wao hivi: Sasa nitawauliza, wanaoafiki waseme ndiyo. Utasikia wengi wenye chama chao wakijibu Ndiyooooooooooooooooo. Watauliza wasioafiki wasema siyo. Watajibu Siooooooooooooooooo.
Mnajua akitakachotokea. Spika wa Bunge hilo atasema, nadhani walioafiki wameshinda. Huo ndiyo unakuwa mwisho wa mchezo, tunasubiri tu referendum!
Msiojua kinachokuja hivi ndivyo itakavyokuwa. Hivyo tusiposhinikiza muswada uletwe bungeni kama ilivyoahidiwa naWaziri Mkuu, basi tujue sisi wenyewe tutakuwa tumebariki iwe hivyo wanavyotaka waliotaka wakati kwenye ilani yao ya uchaguzi 2010 hawakuwa na kipengele cha Katiba mpya.
Kazi kwetu, kusuka au kunyoa. Binafsi najisikia huru kutoa hili moyoni kama kukumbushia.
Wenu Nikupateje