Hell is real
JF-Expert Member
- Aug 14, 2021
- 204
- 364
Ninachojua aliyemtakatifu 666 haimuhusu!!! Ila 666 inamhusu yule ambaye atabaki baada ya unyakuo, na hata kama chanjo ingekuwa 666 mimi inanihusu nini kwa sasa, kwa sababu haiwezi kufanya kazi mwilini mwangu, biblia inasema yaliyofunuliwa ni ya kwetu yaliyofichwa ni ya Mungu, mm naenda kuchanjwa kama chanjo ya kawaida surua, nk kama kuna vyitu vingine vimewekwa kwa siri kimsingi haviwezi kufanya chochote mwilini!
Mbona hilo haliitaji nguvu nyingi kulijua, hivyi kweli angekuwa sio Mungu anayetupingania na vyitu vingi tusivyoviona leo wengi tungekuwa tulishakufa siku nyingi sana, Yesu anasema mtakula hata vyitu vya kufisha lakini havitawadhuru!! Kitu ambacho tunatakiwa kujua ni kwamba aliyemtakatifu hamna kitu kibaya chochote kitakachoingia mwilini mwake kikafanya kazi!
Mfano mdogo bidhaa nyingi tunazozitumia nyingi zenye serial number ni mpinga kristo yaani 666, na wengi humu huwa tunaenda supermarket kununua hivyi bidhaa na zinafanyiwa scanning, unachotakiwa kujua ni kwamba dunia ya sasa hivyi kila kitu kilishaningia kwenye mfumo wa 666 hata hapa Tanzania tulishaingia Siku nyingi, yeyote anayetumia NIDA, account number ya benki, Tin number, yote hii ni mifumo ya 666, isipokuwa haiwezi kufanya kazi kabla ya unyakuo!
Sasa nawashangaa watumishi wa Mungu mnakomaa na chanjo ya corona badala muamazishe watu wajitakase Yesu anarudi kuchukua kanisa, aliyemtakatifu hii 666 kwa sasa haiwezi kufanya kazi kwenye mwili wake kwa sababu haijaruhusiwa, kinachofanyika kwa sasa shetani anaweka mifumo ili ule mda ukifika ni swala la kuanza tu kutekelezeka haya ya sasa ni maandalizi, kumbuka ni mda wa miaka 7 tu atatawala dunia mpinga kristo ndo maana maandalizi lazima anafanya kipindi hiki, wewe uliye wa Mungu unatakiwa uchangamke na kukesha kwenye maombi ili usije ukaachwa!!
Jambo la pili Mungu hapendi kifo cha mtenda dhambi, ndo maana anawanyeshea mvua wema na wabaya! Hivyo kama wewe ni muombaji au ni mtu wa ibaada unaweza kuomba malaria ikakuacha au corona isikupate jua kwamba kuna mwingine ambaye hamjui Mungu wala Hajui hata kuomba, na Mungu anamtaka aishi ili siku moja akatubu na kumgeukia muumba wake, wale ndo ambao Mungu analeta chanjo kwa ajili yao analeta vidoge kwa ajili yao, kumbuka yule malaya anayejiuza Mungu anampenda aishi, mwizi, mzinzi, mwasherati, waabudu sanamu nk,
Hivyo kama wewe umejaliwa kuomba na kudumu katika ibaada usijiinue ukijiona bora kuliko wengine, hicho ndo tunakiita kiburi cha Uzima!!, biblia inasema tusijione bora kuliko wengine bali kila mmoja aangalie mambo ya wengine, wewe umepata neema ya kuabudu na kufunga na kuomba Mshukuru Mungu, sio kuwasema wenye imani ndogo.
Yamkini kiwango ambacho wewe unasema unamjua Mungu hata 20% haujawahi kufikia kumjua Mungu, kuna watu ambao walimjua Mungu mpaka kushusha moto, wengine walienda mbinguni bila hata kufa!! Sasa wewe usijifune badala ya kuwasema watumishi wenzako ungeingia kwenye maombi kuwaombea Mungu awasaidie!!
Maneno ya kwenye mitandao hayawezi kumbadilisha mtu!! Anayeokoa na kumbadilisha mtu ni Mungu tu kupitia maombi, Wacheni wanaochanjwa wakachanjwe hiyo ni imani yao, wewe Ambaye una uwezo wa kuomba na kujikinga kwa namna hiyo ni sawa pia lakini tuache malumbano ya kijinga, tutumie hekima zaidi huku tukijifunza kwa waliotutangulia akina paul, hanna sehemu walisemana, hata Yesu mwenyewe alisema asiyekinyume Chetu ni mwezetu!
Naamnin kipindi hiki cha mwisho naomba tuwe makini sana na Roho zidanganyazo wapendwa, kaa kimya Tafakari tumia hekima na Muombe Mungu ili maneno yako yasije yakawakosesha hata hawa walio wadogo!!! Mungu awabariki sana,