SoC02 Tusipuuze fursa za kimtandao

SoC02 Tusipuuze fursa za kimtandao

Stories of Change - 2022 Competition

Br Joseph Chacha

New Member
Joined
Aug 27, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Ndugu, wanajamii Forum na wasomaji wote, kumekuwa na wimbi la watu wengi hasa vijana tunaotumia mitandao ya kijamii kwa wingi kupuuza frusa zitokanazo na mitandao ya kijamii. Hii ni kutokana na wimbi kubwa linalozuka katika mtandao juu ya utapeli wa kimtandao, watu wamepoteza imanai juu ya frusa zitokanazo na mtandao, watu huishia kukejeri ama kupuuza tu frusa hizo.

Mfano mzuri ni shindano hili, yawezekana wengi hawana hulks ya mashindano ya aina hii , lakini tizama comment zao utajua kuwa ni watu wasiokuwa na Imani juu ya frusa za kimtandao kwakuwa aidha walishatendwa kimtandao kwa kuibiwa yaani kuibiwa au hawana imani na vyombo husika vya kuendesha mashindano au frusa hizo za kimtandao.

Nakumbuka watu husema katika mashindano ya aina hiyo wahusika huwa wanajichagua na kushinda wenyewe, ama kuna njia zenye mizengwe na vitimbwi katika kupata washindi.

Mimi najitokeza kuwahamasisha tusipuuze frusa za kimtandao kwani kila mtu ana kudra yake, kujaribu inatupasa, kwani mkeo akipata ujauzito ukatoka ama akajifungua mtoto akafariki huwa kikomo cha kumsaka mwana mwingine? Ama chuoni ukipata sapu hurudii mtihani ili uende mbele? Kikubwa ni kumakinika kwa vigezo vya frusa hizo ili kuchekecha akiri kujua mbivu na mbichi.

Kumbe tunahitaji kuwa na uthubutu kutumia frusa za kimtandao kwa maendeleo chanya ya binafsi na jamii. Kufanya hivyo kutasaidia kuepuka kutumoa mitandao kwa uhalifu na kumomonyoa maadili ya kizazi check kizuri cha Afrika.

Himahima tubadilike, tusipuuze frusa za kimtandao, mimi nimethubutu sasa nizamu yako.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom