#COVID19 Tusiruhusu Covid-19 iathiri uchumi

#COVID19 Tusiruhusu Covid-19 iathiri uchumi

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
426
Reaction score
685
Julai 25, 2021 Wizara ya Afya imetoa muongozo wa kiafya ambao kimsingi haujaangalia ukali wa COVID19 na hali za maisha ya watu mtaani. Eti kinyozi anunue mataulo... ekhe wakati yeye vinyozi tuliozoea hata kubadili wembe ni ishu, hiyo mashine yenyewe kaiunga unga, ya moto hata mwenyewe inamuunguza ekhe..

Naongea kwa data
Kwa data ambazo nimezichukua kutoka Worldometer na kuzifanyia analysis ndogo kabisa, hadi sasa watu waliopimwa COVID19 ni 2,952,624,180 waliokutwa na maambukizi ni 194,843,917 ambayo ni 6.59% kwa maana yake ni kuwa hata hizi wanazosema kuwa maambukizi ni makubwa kiuhalisia si kweli kwa kuwa ni sehemu ndogo ya wanaopimwa hukutwa na maambukizi

Katika hao wenye maambukizi 90.73% hupona wakati vifo ni 2.14%. Huku watu ambao bado ni wagonjwa ni 7.12%. Katika watu waliogundulika kuwa na maambukizi dunia nzima 0.6% hadi leo (Julai 26) ndio wako mahututi.

✍️NB: Najua hapa nakuwa naongea na watakwimu zaidi kwa kuwa asilimia ni muhimu kuliko idadi

Hivyo basi, Twimu hizi zinaonesha maambukizi yako chini kuliko tunavyoaminishwa, vifo viko chini kuliko tunavyoaminisha, na walio mahututi ni wachache. (Hii sio kusema kuwa ugonjwa haupo)

Ndio sababu hadi sasa mbali na maisha yetu ya kujiachia nchini, bado hakujawa na vifo kiasi cha kuokota maiti mitaani, watu wanaendelea kuishi bila shida

Uchumi wa nchi
Mwaka 2019 na 2020 uchumi ulikuwa mzuri kwa kuwa tulipuuza kila kitu na mambo yakaendelea kama kawaida. Mwaka 2021 tumeanza kuchukua hatua ambazo moja kwa moja zinaathiri uchumi na kwa kiasi kikubwa

Note👉 Corona haiathiri uchumi, ila hatua tunazochukua kukabiliana na corona ndio zinaathiri uchumi

Hatua kama kuzuia, matamasha, sherehe, michezo, nk. Ajira za maMC, maDJ nk zimeathiriwa moja kwa moja. Watu wengine watapata madhara kutokana na shughuli zao kwa namna yao pia. i.e Masharti ya masokoni na kwenye minada ni kichekesho kingine

Madhara zaidi
Watu watatakiwa kuongeza gharama ya maisha ili kununua vifaa zaidi, i.e maji, sanitizers, barakoa nk. Maji na Sabuni, sanitizers ni gharama kwa wafanyabiashara ambao wanalazimika kuwa na vitu hivyo kwa mujibu wa sheria. Msishangae kuona benki ziliacha kuweka sanitizers kwenye ATMs kipindi fulani, the truth is hiyo kitu ni gharama kwao. Pia kuna watu wametakiwa kuwa na vitu vya kupimia joto la wateja, kichekesho kingine.

Suluhu ninayoiona
Kwa kuwa uongozi unataka kutoa chanjo kwa kuwa tayari hela za kupambana na COVID19 zimeshachukuliwa, basi nashauri watu wachanjwe kama ambavyo waliotoa hela wanataka, kisha maisha yaendelee kama tulivyozoea bila kuathiri uchumi ambao ndio kwanza tuko Lower Middle Income Country

Kwenu viongozi
Viongozi wa nchi hii, mjue kuwa katika nchi ambazo mnadhani wanachukua hizi hatua hali imeshakuwa mbaya na watu wanagoma na kuandamana kila uchao kupinga viu ambavyo mnavileta nchini. Kwa habari za watu kugoma na kupambana dhidi ya chanjo, lockdown na vitu vingine naomba mtembelee ukurasa wa Habari wa Urusi t.me/rtintl (Telegram channel)

Zaidi Ndugu zangu tuwe na analysis kubwa za kila ambacho tunakisikia duniani

Nawasilisha

Signed OEDIPUS
 
Huo ni muongozo tu, kwani ni lazima ufuatwe?
 
Back
Top Bottom