Tupo karibu sawa na Nigeria ambapo tumewazidi kidogo sana.
Nigeria kwa uwingi wa watu ni mara 3 na ushee zaidi yetu. Kupata ardhi ya kujenga ni mtiti haswa na wengi wa maisha ya kati wanakimbilia kujenga kwenye asili yao na kununua flats miji mikubwa kama Abuja na Lagos.
Lengo ni kusema, zile nchi 5 za EA haswa, nne zilikuwa na lengo moja la kuiteka ardhi ya TZ kwa manufaa yao. Mu7 akiwa m/kiti kwa kushirikiana na PK sio! Kenya wao wakiwa jeshi la mtu mmoja. Sasa wamewatamanisha na akina Burundi, Sudan na hata Malawi naye kaanza kututolea macho.
Sasa hawa wote kwa ujumla wao, wakifunguliwa milango, nini kitatokea? Ni kama tunavyoona sasa, koti limeshaanza kubana, ila wanasema tumeshaingiliana sana, itakuaje tukimwagana? Ingawa ukweli ni kuwa TUMEINGILIWA sana, si wanamiliki ardhi na kila kitu huku, vipi sisi kumiliki kitu kule?
Ndo yanayoenda kutokea, Wakenya watamiliki ardhi na kila kitu huku wakiwaambia hamruhusiwi kumiliki chochote kule, wale wasomi na wenye ujuaji mwingi waendelee tu kutuelewesha KWANINI HATURUHUSIWI KUMILIKI ARDHI HAPO ZNZ ila iwe rahisi kumili KENYA?