Tusisaidie hizi shule kupata matokeo ya ushindani

Mzee Mwenzangu

Senior Member
Joined
Dec 23, 2013
Posts
190
Reaction score
168
Habari wana jamvi.

Naomba kwanza nieleweke kuwa naandika haya kwa nia njema.

Ukifuatilia shule nyingi chini ya mwamvuli wa dini ya kiislam hazifanyi vizuri. Naomba tujadili ni ni kikwazo ili miaka ijayo nazo ziwe katika shule shindani na watoto wetu waweze kujivunia kusoma hapo.

Najua shule haichagua mwanafunzi (kidini) hivyo kama shule nyingi especially hizi za dini zote huwa zina maadili ambayo ni msingi mzuri kwa wanetu na ningefurahishwa nazo zote zikiwa zinashindana ktk hizi nafasi bora kitaifa.

Tupia nini kifanyike au tujifunze kutoka shule za wakristu ili tuwe katika ushindani wa kimaendeleo.

Nami nitarudi baadaye kuchangia baada ya wadau kutupia maoni.

Karibuni.
 
MMhhhhhhh udini utaibuka hapa!.... Ajiri waalimu toka dini zote.. na tena msilipe kwa ubaguzi wa kidini.
 
umeangalia matokeo ya NYASAKA ISLAMIC SEMINARY S1665.waulize wao wanafanyaje mpaka wanakuwa na div 1-35
Div ii-87?
 
MMhhhhhhh udini utaibuka hapa!.... Ajiri waalimu toka dini zote.. na tena msilipe kwa ubaguzi wa kidini.
Nmekupa na like, mie binafsi nmesoma boding kuanzia kidato cha kwanza mpaka mwiso, tatizo la waislam ni ubaguzi, wakati nnasoma walikuwa hawachangamani sana na wakristo je unategemea nini kitokee kama huchangamani na watu?
Sina hakika ila nnaimani hata kwenye taasisi zao hawaajiri walimu wakristo/watu tofauti na maadili yao.
Kikubwa waache ubaguzi wa kidini, wajaribu kumchukulia kila mtu jinsi alivyo...........
 
Kama wanavokazania madrasa,wakazanie pia elimu dunia watafanikiwa tu...shule za catholic kwa mfano church mnasali sanaa tena kwa bidii na shule mnasoma sanaa as well,.
Kuandamana NECTA hakutawasaidia..WASOME KWA BIDII,pia waache kuita watu wengine makafir,
 

like,kweli kabisa me nishaiona hii wkt nasoma shule flani hivi o level,wanapangiana group discussion masjid,af group leader unakuta sio mkali kivile,
wajifunze kuchangamana
 
like,kweli kabisa me nishaiona hii wkt nasoma shule flani hivi o level,wanapangiana group discussion masjid,af group leader unakuta sio mkali kivile,
wajifunze kuchangamana
Walikuwa wanahamishia magodoro masjid.
 
Ishukubwa ni kubagua wanajamii walio kinyume na maadili na dini namaanisha walimu na wanafunzi. nadhan waajiri walimu wazuri bila kujari dini na hata wanafunzi pia then wawape uhuru wa kuabudu na kuishi kwa imani zao kama inavyofanyika kwa shule za din za kikristo. Mie nadhan watafanikiwa tu ila kinyume na hapo itakua iviivi miaka yote na kutafuta mchawi wizaran na NECTA
 
Naombeni matokeo ya Gogoni Sekondari over roll na mwanangu na feza boys ilinijue atakuwa group lipi

Ndo nijadili
 
Soma na matokeo ya Maawal Islamic secondary walivyopasi,hii shule kipindi cha nyuma ilikaribiya kufutwa.Walibadili uongozi,inafanya vizuri sasa.
 
Tuache bangi jaman,hayo mambo ya nin?
 
Nimeangalia maoni ya wengi, asilimia kubwa wametushauli kuajili waalimu wazuri na kuacha ubaguzi.
Kuna shule zenye maadili ya kiislam ambazo nimeshauriwa nijifunze kutoka kwao, nitajaribu kufuatilia wamewezaje kutoka.
Labda kwa wale wenye nia ya dhati ya kusaidia, tujaribu kuangalia sehemu tunazoishi, kuna ile kitu tunaita mabaraza ya shule, wale wanaoongoza na wanachama wengine wa baraza hilo ni watu wenye mlengo wa elimu?
Ambacho naona wakatoliki wameweza kufanikiwa ni kuzifanya shule zao nyingi kuwa za kulala, na ninaamini hata hizo shule za kiislam nilizoambiwa nijifunze kutoka kwao ni za kulala (sina uhakika). Je kulala kuna muongezea mwanafunzi umakini wa kuzingatia masomo? au kipi tena cha ziada?
Bado nasisitiza kuwa shule zoe zenye mlengo wa dini nazipenda sababu ya maadili kwa watoto wetu

Karibuni
 
Wanaomkana Yesu kwa kusema "Yesu si Mungu ni makafiri" soma Yud 1:4.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…