Tusitafute mchawi kwa anguko la elimu tz

KESSY FRANCIS

Member
Joined
Nov 9, 2011
Posts
42
Reaction score
11
TUSITAFUTE MCHAWI KWA ANGUKO LA ELIMU TZ
Wanasiasa uchwara, wanaharakati, na makuadi wa magharibi kwa pamoja wamekuwa wakiendeleza body language za walimu wanaonewa, elimu mbovu,walimu wanahali ngumu, Haki zao hawapati. Umekuwa wimbo wa kila siku bila kutafakari kwa kina matokeo ya maneno hayo kwa WALIMU, na WANAFUNZI. Ni kweli tatizo katika sekta elimu aijaanza leo! Toka uhuru lakini TUSITAFUTE wachawi ni sisi. Tumefifisha moyo wa walimu kwa mda sasa kwa maneno yasiyokuwa na UWAJIBIKAJI. Mbona shule zenye maabara za kisasa, walimu wa kutosha, wenye mishahara mikubwa kuliko serikalini wamefeli tena kuzidi shule zingine za KATA licha ya matatizo yake zimefaulisha!!. Tatizo hapa ni MAADILI. Sekta ya elimu inakabiliwa na ugonjwa wa KUSHUKA NA KUZOROTA kwa MAADILI. Wanafunzi hawana maadili sambamba na WALIMU wao. Kuna baadhi ya kazi zinafanywa kwa ethics tu, ikiwemo ualimu, uuguzi n.k. Matatizo ni mengi lakini kubwa ni MAADILI, mengine yanafuata, mbona wakati sisi tunasoma hapakuwa na maabara, wala library, na hata walimu hawakuwepo wa kutosha lakini hatukuchora MESSI na kutukana kwenye makaratasi ya kujibia. Leo hii tumemaliza vyuo!! Na tupo makazini. Tusishabikie matatizo yanayowakumba walimu kwani kufanya hivyo ni kushiriki kuua taifa na vijana wake. Tusikubali kuwa sehemu ya matatizo Bali kuwa sehemu ya majawabu
 
::
Wenye maadili hawana madaraka na wenye madaraka hawana maadili.
=
 
Sasa tunafanyaje??

::
Hakuna njia moja ya kutumia ila mwl Nyerere aliwahi kusema ukiwa na matatizo mengi kama miguu ya jongoo UNATEMBEA TU itajipanga.
Kwa kuwa maadili ni roho na roho iko polluted..tuanze kutembea (kutatua) tu kwa tutimize tu pasipo kutegemea hisani
=
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…