Tusiwakejeli watuhumiwa

Tusiwakejeli watuhumiwa

Exaud J. Makyao

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2008
Posts
1,518
Reaction score
24
MIMI NI MMOJAWAPO WA WATANZANIA WANAOPENDA KUONA NCHI YETU INAONGOZWA NA VIONGOZI WAADILIFU KABISA.

LAKINI NASHAURI TUSIWATANIE NA KUWAZOMEA, NA KUWAKEJELI WALE WANAOTUHUMIWA KWA KUTOKUWA NA UADILIFU.

NASEMA HIVYO KWASABABU, ''MTUHUMIWA SI MHALIFU'' HADI PALE SHERIA ITAKAPOMTIA HATIANI.

NASHAURI TUSIWAKEJELI KABISA KWA KUWA BADO NI BINADAMU WENZETU NA SHERIA HAIJAWATIA HATIANI.

Exaud J. Makyao
0784347001
 
Inategemea mwenendo wa mtuhumiwa kabla ya tuhuma.Kama alikuwa ana mwenendo unaokera au kuumiza wengine basi atakapokuwa anatuhumiwa, kejeli zitakuja tu maana hulka ya binadamu ndivyo ilivyo.Mbona kuna watuhumiwa chungu mzima hawakejeliwi? Hao wanaokejeliwa basi kuna jambo!
 
Ukumbuke kuwa watuhumiwa ni watu waliowakejeli sana watanzania. Kuna mmoja alisema kwa majivuno, "hata kama watanzania watakula nyasi ndege itanunuliwa" na mwingine aliyaita mapesa "vijisenti". Kama unakumbukumbu nzuri fuatilia waliyokuwa wanaongea bungeni na kwenye kampeni za uchaguzi kwenye majimbo yao, au hata walipokuwa wanaongea na waandishi wa habari, ulinganishe na waliyofanya. Hizo ni kejeli za waziwazi, ingawa wewe unaona ni watuhumiwa(ambayo ni haki yao kisheria) lakini kuna watanzania wengine wanauhakika kuwa ni WAHALIFU na sio watuhumiwa tu. Hili la kuwaita watuhumiwa ni neno la kisheria kwa wahalifu ambao bado hawajathibitishwa na utaratibu wa mahakama
 
Mramba alipata kusema!

-" Acha wananchi wale majani lakini ndege ya rais itanunuliwa tu kwani rais sio Yesu apande punda"
-"Kama daladala zimegoma basi watu watembee kwa miguu kuja makazini"
Makyao kwa hayo machache unategemea nini Mdanganyika wa kawaida anayehaikia mkate wa leo bila uhakika wa mlo wa baadaye afanye nini kwa mtu kama huyo?
Plz let NATURE take its course.
 
Aisee umenikumbusaha hive kweli Mramba alisema "Raisi siyo Yesu apande punda" nasi wananchi wale hata majani bali ndege itanunuliwa tu!!! Kejeli gani hizi ndio maana wananchi wamechoshwa kama haya yalisemwa....
 
what goes arround comes arround! Bwana Makyao habari ndio hiyo
 
Aisee umenikumbusaha hive kweli Mramba alisema "Raisi siyo Yesu apande punda" nasi wananchi wale hata majani bali ndege itanunuliwa tu!!! Kejeli gani hizi ndio maana wananchi wamechoshwa kama haya yalisemwa....

Kilichotakiwa hapa ni ufafanuzi wa maana aliyokuwa nayo Mramba na wala si sisi kuzipatia maana zetu hizo kauli.
 
Back
Top Bottom