Ukumbuke kuwa watuhumiwa ni watu waliowakejeli sana watanzania. Kuna mmoja alisema kwa majivuno, "hata kama watanzania watakula nyasi ndege itanunuliwa" na mwingine aliyaita mapesa "vijisenti". Kama unakumbukumbu nzuri fuatilia waliyokuwa wanaongea bungeni na kwenye kampeni za uchaguzi kwenye majimbo yao, au hata walipokuwa wanaongea na waandishi wa habari, ulinganishe na waliyofanya. Hizo ni kejeli za waziwazi, ingawa wewe unaona ni watuhumiwa(ambayo ni haki yao kisheria) lakini kuna watanzania wengine wanauhakika kuwa ni WAHALIFU na sio watuhumiwa tu. Hili la kuwaita watuhumiwa ni neno la kisheria kwa wahalifu ambao bado hawajathibitishwa na utaratibu wa mahakama