Uchaguzi 2020 Tusiwalaumu sana TBC, Star TV, Channel 10, ETV na wengineo

Uchaguzi 2020 Tusiwalaumu sana TBC, Star TV, Channel 10, ETV na wengineo

kamtesh

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2014
Posts
1,395
Reaction score
513
Nadhani walibanwa mno, na ukiangalia uongozi wao utajua kwanini? Hata nyuso za watangazaji, ilikua unaona kabisa hawana raha kushindwa kutangaza taarifa za upinzani.

Ilikua unaona kabisa nini kilichikuwepo nyuma ya pazia. Hata NEC haikukemea vyombo vya habari hususani Runinga kushindwa kutangaza kwa ufasaha taarifa za upande wapili. Hata radio, zilishindwa ndo maana CCM wanachukia sana mitandao ya kijamii. Leo lao lilikua wapinzani wasionekane popote, ili wao wawe wao tu.

Azima yao haijafanikiwa ya kufuta upinzania nchini, kinyume chake, upinzani umekuwa na nguvu zaidi kuliko walivyotemea. Ndo maana walipitisha visheria vingi kandamizi vya kukandamiza mitandao ya kijamii.

Kwahio hivi vyombo vilivyo shindwa yakiwemo magazeti, wengi wao ilikua uongozi, na pili ilikua uoga. Tuwape pole sana, ila kwakuleta uhondo next time, wachague Uhuru.
 
Hawastahili pole yoyote ile kwa kuamua kwao kwa makusudi kabisa kuweka pembeni weledi wa kazi yao na kuchagua kutumika kwa manufaa ya kisiasa. Unafiki na uoga walio uonesha kwenye uchaguzi wa mwaka huu, umewadhalilisha na kuwadharaulisha kwenye jamii ya Wapenda Haki kwa kiwango kisicho elezeka.

Walishindwa nini kuwaiga Watumishi wa Umma ambao kimsingi wamekubali liwalo na liwe kwa kuweka dhamiria ya kutompigia kabisa kura Mgombea anayemaliza muda wake baada tu ya kuwafanyia madharau, kejeli, kiburi na kila aina ya manyanyaso, usumbufu na vitisho kwa miaka yoye hii mitano!
 
Nadhani walibwanwa mno, na ukiangalia uongozi wao utajua kwanini? Hata nyuso za watangazaji, ilikua unaona kabisa hawana raha kushindwa kutangaza taarifa za upinzani...
Ila hii ni aibu kwa CCM. Yaani chama kizee kina waogopa upinzani kiasi hicho.
 
Ni aibu ya Karine na wanajipambanua sana kwamba wanapendwa na wala wanachama milioni 16 sijui kwa takwimu zipi hizo maana ccm haijawahi shinda kura zaidi ya milioni 10 hata siku moja.
 
Usiwatetee hakuna aliebanwa ,aliebanwa hujiuzulu,dunia ikafahamu uwazi. Mbona habari za Ntwara awatuletei atujui mapigano na alishababu yamefanikiwa au bado tunawatwanga ka tulivyomtwanga Idi amini
 
Utawala wa Magufuli unasikitisha, unahuzunisha, unapandisha hasira.

Tuombee Mungu watu wasiingie barabarani ila wakiingia haki ya Nani magu ataiona Tanzania chungu na hata amini.
 
Zile ruzuku, michango ya wabunge, mngezitumia vizuri kujenga saccos yenu badala ya kujenga tumbo la mwenyekiti wenu. Chama hakina mbele wala nyuma ndio leo mnataka ridhaa kwa watanzania mmechemka vibaya mno. Mbowe kaua chama mchana kweupe. Kuja kulialia humu kunazidi kuwavua nguo.
 
Hakuna chombo cha habari kitaenda kutega maiki yake kutoka kwa msaliti wa Nchi anayeropoka matusi
 
Umeandika utafikiri hao wanafanyia kazi watu bure.. mnataka sana vya dezo dezo.. kaongeeni kwa zile za huko majuwuuuu..

💛💚💛💚💛
 
Back
Top Bottom