#COVID19 Tusizuiwe kuwaza nje ya box kuhusu chanjo ya corona

#COVID19 Tusizuiwe kuwaza nje ya box kuhusu chanjo ya corona

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2011
Posts
1,684
Reaction score
2,156
Tangu Rais atangaze kuruhusu chanjo kuingia nchini limeibuka wimbi la mchanganyiko wa mitazamo juu ya ubora na uthabiti wa chanjo yenyewe

Watanzania wengi ni Kama hawajaridhika na yanayosemwa juu ya ubora wa chanjo hiyo kutokomeza corona.

Kutokana na mtazamo huo, wameibuka watu wa kuhamasisha wengine wachanjwe. Sababu wanazotoa kuelezea usalama chanjo hizo ki ukweli ukizitafakari kwa kina zinaweza zisishawishi kukubaliana nazo

Kwa mfano, wanaokubaliana na chanjo wanasema ni salama kwa sababu na wazungu wamechanjwa hizo hizo. Huu ni upuuzi kuendelea kuamini kwa kila kinachotumiwa na mzungu ndio kitu bora na salama

Pili wanashindwa kutwambia kwanini wimbi la kwanza na la pili halikutuathiri sana Kama walivyoathirika wenzetu (wazungu)!? Kusema kwamba wimbi la tatu la delta ni kali kuliko wimbi la kwanza na la pili haitoshi kwasababu hata hilo la kwanza na la pili lilikuwa hatari sana kwa baadhi ya mataifa.

India , Brazili, Marekani, A.kusini na kwingineko watu walikufa sana! Kwanini hawatupi sababu za kisayansi zinazoonyesha tishio kwa wimbi hili la tatu kwetu

Halafu tena wanasema kwamba hoja za kwamba wazungu wanataka kutumia chanjo hizi kutumaliza ni mfu kwasababu wanazo njia nyingi nyingine wanazoweza kutumia kufanya hivyo

Hapa hata Mimi nakubaliana nao kwa asilimia zote. Wanaosema hii chanjo ya corona lengo ni kuangamiza Afrika nao wanabuni tu na hawajui hata wanalosema.

Hoja yangu katika hili ni kwamba hii chanjo inapigiwa debe sana kwasababu za kibiashara zaidi.

Kama mnakumbuka G7 walikaa wakakubaliana kwamba wachanje watu wao halafu watoe 20% ya chanjo za msaada kwa nchi masikini. Yaani asilimia 80 ya watu watagharamikiwa na serikali yao wenyewe!

Bara la Afrika na dunia limesumbuliwa na magonjwa ya HIV, TB, MALARIA, Cancer na magonjwa mengine mengi kwa miaka mingi. Kwanini haikuwahi kutafutwa chanjo za magonjwa haya kwa dharula Kama ilivyofanyika kwenye corona!?

HIV inaenezwa na virus anayebadilika badilika kila mara hoja ambayo imekuwa ikitolewa na wanasayansi kwamba ndio sababu ya kukosekana kwa chanjo na dawa ya gonjwa hilo. Wamewezaje kwenye corona inayobadilika badilika Kama HIV!?

Swali la msingi, hii chanjo imetengenezwa kwa kutegemea tabia za virus wa mwanzo. Sasa je, inaouwezo wa kupambana na aina nyingine za virus wa huyu Corona anayebadilika badilika!? Kama wameweza kwanini kwenye HIV wameshindwa kwa miaka yote hiyo!?!

Wanasayansi na wanasiasa wasizuie watu kuwaza nje ya box kuhusu chanjo hii. Waje na majibu ya maswali haya ili kutoa Elimu na kujenga uelewa kwa watu.
 
'
20210731_155359.jpg
 
Turuhusiwe kuwaza namna ya kugundua Chanjo yetu Watu weusi,Babu wa Loliondo alipokuja na 'Kikombe' sikuona wapingaji kwa kasi hii nimewaza labda kwasababu ilikuwa ni fubu.
 
Back
Top Bottom