kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Kuna njia kuu mbili za kujifunza na kurekebisha mambo yako'; kujifunza kwa kutumia makosa yako mwenyewe au kujifunza kwa kutumia makosa ya wengine.
Kenya wanataka kumuondoa Makamu wa Rais wao Mh. Gashagua kwa makosa aliyotenda akiwa Makamu wa Rais; Je, makosa wanayomtuhumu nayo sisi hatuna viongozi waliofanya makosa hayo tangu 1961 tulipopata Uhuru hadi sasa? Kama walikuwepo Je, viongozi hao tuliwafanya nini? Je, viongozi wetu wajifunze kutoka Kenya kuepuka kufanya makosa kama wanayohangaika nayo Kenya au waendelee kufanya makosa ili tuwahukumu kama wanavyofanya Kenya?.
Ni kweli hatuna viongozi wanaopokea zawadi bila kuzitangaza na kuzikabidhi kwa umma?
Ni kweli hatuna viongozi wanaopendelea maendeleo ya kwao na watu wa kwao?
Ni kweli hatuna viongozi wanaoingilia michakato ya tenda?
Ni kweli hatuna viongozi wa umma wanaotumia ofisi za umma kwa maslahi yao?
NI kweli hakuna viongozi ambao wanaficha miradi/mali kwa kutumia watoto na wake zao (conflict of interest)?
Tunangojea nini kuwahoji viongozi wetu wenye mali zisizofanana na kipato chao?