Uhuru24
JF-Expert Member
- May 2, 2015
- 4,112
- 4,361
Mtaa wa Lindi na Shauri moyo kuna hiz taaa za trafic light jirani kabisa na stand hii kubwa ya mwendo kasi, cha ajabu hizi taa zinasumbua inakimbilia mwez sasa hazifanyi kazi. Sasa cha ajabu kuna muda zinafanya kazi zinapoamua ila ufanyaji wake wa kazi ni wa vichekesho wa hali ya juuu.
Wote tuliopo mijini tunajua jinsi hizi taa zinavyofanya kazi, kwamba zinazuia huku na upande wa pili zinaruhusu magari kuendelea na safari(yaaan kwa zamu) cha ajabu hizi taa zinapojisikia kuwaka basi zinawaka zote kwa mara moja, kama nyekundu zinawaka zote taaa kuanzia njia kubwa, watembea kwa miguu, na za njia panda, na ikiamua kuwaka kijani nazo hivyohivyo zote zinawaka, sasa hofu yangu nikwamba zinapowaka za kijani, aliyepo njia kubwa atakuja kwakasi, na aliyepo njia za mchepuko(njia ndogo) nae atakuja kwa kasi nae hapo ndipo ajari itakapotokea.
Wahusika wafuatilie maaana siku ya leo ndio zimeamua kuleta vibweka kwelkweli