Tutaangalia mpaka lini?

Bin Maryamu, nani kasema hatuna resource au hazitoshi? Sidhani kama tatizo ni resources, tatizo kwa maoni yangu ni watu wanaosimamia resources hizo.

Ni rahisi kuziba ufa kuliko kujenga ukuta. Tungeingilia kati Rwanda mapema tusingelipa gharama kubwa ya kuhudumia wakimbizi. The same applies to Kenya, tutalipa gharama kubwa ya kiuchumi na kijamii kama Kenya itaingia kwenye machafuko makubwa zaidi kuliko gharama ya kuingilia kati sasa.

Nina uhakika, tukija na mpango mzuri jamii ya kimataifa watakuwa tayari kusaidia.
 

Na bado wanaendelea!
 
umuhimu wa kusaidia kuepusha upotevu wa maisha ya ndugu zetu wa Kenya ni muhimu sana. hata hivyo ni muhimu kuangalia kwa makini njia muafaka ya kuhitimisha lengo hilo.

sidhani kama tanzania kuingia kijeshi na kusidia kutuliza amani ni rahisi kwani itabidi serikali yetu ipate kibali cha kufanya hivyo kutoka serikali ya Kenya (Kibaki?). Je, Kibaki akiomba msaada wa aina hiyo tanzania itautoa? Je, kwa kufanya hivyo haitaleta tafsiri ya kuitambua rasmi serikali ya Kibaki na hivyo kuonekana kuchukua moja kwa moja upande katika mgogoro huo?

Labda Tanzania tuitwe na wahanga wake (Kibaki na Odinga). Likifanyika hili pande zote mbili zishauriwe kukubali kuweka maeneo salama ambapo wananchi walioathirika au wanaotishiwa usalama wao wapate pa kukimbilia. Maeneo haya salama yanaweza lindwa na jeshi la kenya (kama wananchi bado wana imani nalo) au majeshi ya nchi rafiki wa kenya. Hii itaondoa uwezekano wa kufumuka tatizo la wakimbizi.

Mara nyingi nchi zinazopaka husita sana kupeleka jeshi katika nchi jirani kwa kuogopa kumezwa na kufanywa sehemu katika mgogoro
husika. Aidha kama nchi hizo jirani zinafanana nguvu zao za kijeshi hapo ugumu huongezeka. Kama mkataba wa EAC ingekuwa na kipengere kinachoruhusu nchi wanachama kuingia kijeshi kuokoa maisha ya raia iwapo mwanachama yupo matatizoni basi ingekuwa rahisi kwa tanzania kuingia kenya kama eac na sio Tz. Hata matatizo ya Serbia/Kosovo majeshi yaliyotumika ni nato na sio Ujerumani au Marekani japokuwa ndege zilizoangusha mabomu ni za wamarekani.
 

Nimeitoa BBC leo. Tutamrudishaje jini kwenye chupa?
 
Something kuliko hii apathy! Tik tok tik tok tik tok! Tusije tukasema hatukujua ndiyo maana hatukufanya kitu. Tik tok tik tok tik tok.

..fundi,kujua tunajua sana. hatuna uwezo na mbaya zaidi hatuna nia dhahiri.
 
Uchumi wa Tanzania hauwezi kuwaathirika kabisa na matatizo yanayotokea kule kwa sababu zifuatazo. Sekta kubwa ya uchumi ni misaada na Kenya sio nchi inayotusaidia. Sekta inayofuatia ni madini, migodi iko mbali na Kenya.

..blue band tutaikosa kidogo, lakini tanbond si tunayo!

..omo,foma ipo!

..kimbo,mafuta ya alizeti yapo!
 

..kwanza tuingie kwa faida ipi? we are not imperialists!
 
Mwekezaji mkubwa katika haka ka uchumi ketu ni Kenya.

..fundi,mwekezaji mkubwa [wawekezaji wengi is the correct word] ni makampuni toka kenya,ambayo ukweli ni ya kimataifa yenye makao yake pale!ukisema kenya,it sounds like serikali ya kenya!

..kwanza bora yahamie huku kwetu!
 
Mbona watanzania mnataka kuwa waafrika sana kuliko wengine wakati resource za kutatua matatizo yetu wenyewe hazitoshi?

..mtanzania [si huyu humu!] ni mtu wa domo kaya na kujipendekeza [hasa mimi] hata kama hana uwezo wa kutosha na watoto wanalalia kauzu nyumbani ataenda nunulia wa wenzie nyama au kuku alimradi aonekane naye ni mtu wa maana!

..we need to shake up this mentality!
 
nasikia jana odinga kapendekeza majeshi ya kulinda amani yapelekwe kenya. kasisitiza kwamba majeshi hayo yawe ya un ama au na sio ya nchi pekee.

nadhani nimegusia hapo juu kuhusu umuhimu wa jeshi la jumuiya na si la nchi.
 

Kweli tupu DaRiSalamu. Hiyo dhana ya Tanzania (pekee) kuingilia mgogoro wa jirani, hata kama ni kwa kukaribishwa halifai. Ikiwa ni sehemu ya jeshi la kimataifa, hapo tunaweza kuchangamkia.

Badala ya kulialia na athari za kiuchumi tutakazozipata kutokana na matatizo haya ya Kenya, tungekuwa wakati huu tunapanga mbinu za kuondokana na utegemezi wetu mkubwa kwa Kenya. Badala ya kungoja watalii washukie Kenya kwanza ndio wateremke Tanzania, wakati huu tungekuwa tunaimarisha sehemu zinazofanya hao watalii wasije moja kwa moja Tanzania. Gharama za kupeleka hao wanajeshi huko Kenya zinatosha na kusaza kulitimiza hilo.
 
Kwa wale wanaotaka tunyamaze tu, tukumbuke haya:


Based on a speech by Martin Niemöller on January 6, 1946.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…