Tutachimba mafuta, lakini tuko tayari?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Tutachimba mafuta, lakini tuko tayari?



Kampuni ya Shell kutafiti na kuchimba mafuta Zanzibar. Je nchi iko tayari?

Na Ally Saleh. JUZI tulipata taarifa kuwa hatimae Rais wa Zanzibar Dk Ali Muhammed Shein amesaini mkataba wa utafiti na pengine hatimae uchimbaji wa mafuta na kampuni ya kutoka Uholanzi. Hatua hii tulikuwa tukiisubiri sana na naweza kusema zaidi ya sana. Hapa si pahala pa

kurudia misukosuko na mashaka ya uchimbaji wa nishati hiyo ambayo sio tu ni muhimu ila pia ya lazima kwa maendeleo na uchumi wa Zanzibar.

Hakuna popote pale duniani ambapo nishati hii haikuweza kubadilisha watu wake, ingawa kuna baadhi ya sehemu petrol na mazao yake yote yanayopatikana yamekuwa na laana kwa nchi hizo.

Lakini hizo si nchi nyingi na kwa hivyo si mifano ya kugopa lakini ni mifano ya kuichukulia tahadhari kubwa kwa sababu inaweza kuwa ya maumivu makubwa kwetu na vizazi vijavyo.


Kwa hivyo wakati tukianza kujiweka sawa na suala zima la uchimbaji wa mafuta jambo la kwanza kabisa ni kujitayarisha kwa miundo mbinu ya uchimbaji mafuta salama na wa maslahi na watu wetu.

Ni ushauri wangu kwa hivyo kama ilikuwa hatujaanza basi tuanze haraka kutandika mipango na miundo mbinu ya kuhakikisha kuwa rasilamali hiyo inakuwa ni ya Wazanzibari wote na tusianze kama ilivyoanza kutokea Mtwara au Ogoni au kwengineko.

Pili ni wakati huu ambapo tunapaswa kujitayarisha kwa mambo yote yanayohusu uchumi na uwekezaji wake ambao ni suala la umuhimu mkubwa na tuna mifano mingi ya kuiga duniani kama vile nchi za Qatar ilivyofanya kwa gesi asilia, au Oman ilivyofanya kwa mafuta na kadhalika.

Pia huu ni wakati wa kujifunza juu ya suala la uwekezaji maradufu ( re investment) jambo ambalo ni muhimu katika kukuza utajiri (generation of wealth) ili kujitayarisha kukuza uchumi na nchi isifadhaike pale mafuta yatapokwisha. Katika hili pia kuna mfuko wa utajiri usio kwisha ( sovereign wealth fund) ambayo hata nchi ya Angola imeanzisha.

Hapa kuna mifano mikubwa ya nchi kama China,Qatar,Singapore, Abu Dhabi na sasa Mauritius ambazo zimepanua na kujichimbia kiuchumi kwa kuzua mashirika kadhaa ya kiuwekezaji ya kitaifa kwa maslahi ya nchi.

Mashirika ya ndege kama ya Qatar, Singapore; makampuni ya uwekekezaji kama tunayoyaona yanachipuka huko China yote ni matunda ya faida zinazotokana na gesi au petroli lakini fedha zinarudishwa kwa wazalendo kukuza uwekezaji.

Nimekuwa na fikra inayofanana na hiyo kwa muda mrefu. Na fikra hii ilitokana pia na fikra inayofanana ya marehemu Ahmed Hassan Diria kuwa aliwahi kumshauri Rais Abeid Amani Karume juu ya Zanzibar kuwekeza ndani au nje kwa mintaarafu ya kuwekeza kama nchi.

Leo hivi sasa nalia tena nalia machozi nikiona fursa za kilimo na biashara ziliopo Tanzania Bara ambapo Serikali ya Zanzibar tumeshindwa

kuzichukua fursa hizo. Tulipewa eneo la Makurunge na kama nchi tukazembea sasa Makurunge kuna petroli.

Hivi sasa takwimu angalau za mwaka 2010 zinaonyesha Zanzibar ilifanya biashara na huduma na Bara kwa kiwango cha Billioni Shillingi 125

wakati wenzetu Bara walihitajia kutoka Zanzibar bidhaa na huduma zenye thamani ya Billioni Shillingi 25 tu. Hiyo ni nakisi ya wazi.

Wakati nakisi hiyo haitaki tochi, chembilecho vijana, kuna fursa lukuki Serikali ya Zanzibar inazisinzilia. Hakuna bidhaa yoyote ya Tanzania Bara ambayo imepata wanunuzi wa kutosha kama vile pasivyokuwa na uhakika wa usafiri wa kubeba mazao na kuyaongeza thamani.

Ni wazi kuwa kama Serikali ya Zanzibar ingewekeza katika eneo la kilimo Tanzania Bara naamini ajira kadhaa zingetengezwa kupitia huduma ya usafiri, viwanda na hata utafutaji wa masoko maana alizeti, korosho, mahindi, maharage, tangawizi, zabibu zote hizo zina masoko matamu ya nje.

Pia kama Benki ya Watu wa Zanzibar ingejihusisha katika uwekezaji huko Bara mbona ingekuwa rahisi kupunguza nakisi hiyo ambayo kwa kweli

inaipunguzia Zanzibar nguvu lakini kwa watu wa kawaida wanaona Zanzibar ni kma tegemezi kwa Tanzania Bara.

Kwa maneno mengine inasikitisha kuoana Serikali ya Zanzibar haina mradi wowote huko Bara pamoja na upana wa fursa za kiuwekezaji.

Jambo la tatu la kushauri wakati huu ni lile la kusomesha uinjinia wa mafuta na gesi kwa vijana wetu. Wiki moja nyuma nilimsikiliza Waziri wa Fedha wa Tanzania, akitoa takwimu za usomeshaji katika sekta hizo na kuumia moyoni maana hakutaja hata kidogo juu ya kuipatia Zanzibar wataalamu.

Ni wazi kuwa wenzetu hawatatukumbuka na sisi tunapaswa kujua kuwa toka hapo tuna chumi zinazoshindana basi sasa pia tutakuwa na sekta mafuta na gesi zitazokuwa zinashindana na tusitaraji hata kwa ukubwa wa ukucha kuwa tutapata fursa kutoka kwao.

Ni vyema tuipange ingawa najua kuwa tumeanza. Tuna msingi mbovu wa masomo ya sayansi ni vyema tukajirekebisha na kila ambapo tunaweza tukaazima utaalamu tufanye hivyo. Tusione aibu kutumia uwezo mkubwa walio nao sahibu zetu kama Oman, Qatar, Abu Dhabi maana muhisani wako ndie anaekufaa iwapo jirani hana nafasi.

Chanzo. Tutachimba mafuta, lakini tuko tayari? |

 
Mwandishi anaonekana kushangaa kuona Waziri wa fedha hakutoa nafasi kusomesha wataalam kutoka Zanzibar. Hii ni ajabu, ni ajabu kwa sababu ni wazanzibar hawa hawa waliopaza sauti zao huku wakitoa mapovu suala la mafuta lisiwe la muungano. Ama kweli ukizoea kubebwa miguu husahau kutembea.
 
First things first, mipaka inajulikana? Binafsi sijaona ramani ya Tanganyika wala ya Zanzibar. Issue ya mipaka giza nene.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…