Gmpa
Senior Member
- Aug 1, 2016
- 137
- 45
Mbwa wazaa wengi, wazidiwaje na ng'ombe?
Swali hili ni la msingi, nijibu nipe ujumbe.
Najua hunipingi, wengi ng'ombe wenye pembe,
Wazidiwaje na ng'ombe, mbwa uzaaye wengi?
Mbwa ukizaa sita, ng'ombe mtoto mmoja,
Vipi ng'ombe wakupita mbwa kwenye mchakato?
Mbwa ni wengi mzalipo ni vipi mzidiwe tena?
Mbwa hachinjwi aliwe, useme wanapungua sasa vipi wazidiwe kwa wingi sijatambua,
Wazidiwaje na ng'ombe, mbwa uzaaye wengi
Mbwa ni jibu ulipo, tena kwa sauti pana,
wapi kosa lako lipo, nakuomba nena,
niwengi mzaliwapo, vipi mzidiwe tena?

Mbwa hatua chukua, ili utoe jawabu,
Liweze kutufungua, kujua ipi sababu,
Vinginevyo utakuwa, na kesi ya kujibu,

Sent using Jamii Forums mobile app