Tutaishi kama "Mashetani" ifikapo mwaka 2050

Tutaishi kama "Mashetani" ifikapo mwaka 2050

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Kwa mujibu wa takwimu za sasa za FAO, idadi ya watu wote duniani itafikia bilioni 9.1 ifikapo mwaka 2050, hii ni sawa na asilimia 34 ya ongezeko la ziada ya watu wote waliopo duniani kwa sasa.

Aidha, asilimia 70 ya watu wote duniani watakuwa wanaishi mjini tofauti na sasa ambapo ni asilimia 49 pekee.

Kwa makadirio, Tanzania itakuwa na idadi ya watu wanaozidi milioni 130. Idadi hii ni kubwa sana.

Kwa maoni yangu, ifikapo mwaka huo, Tanzania na dunia kwa ujumla zitakumbwa na changamoto kubwa zifuatazo;
  • Upungufu mkubwa wa chakula, maji na hewa safi
  • Ongezeko kubwa la ukosefu wa ajira zaidi ya sasa
  • Kuongezeka kwa vifo na utegemezi unaotokana na athari za magonjwa ya yasiyo ambukiza
  • Kupanda mara dufu kwa gharama za maisha
  • Kudodoka kwa mfumo wa elimu wa sasa, ambao kwa kiasi kikubwa haulengi kutatua changamoto zilizopo na zijazo
Naona watanzania tunakwenda kuwa na hali ngumu zaidi kuliko sasa. Kama sasa tupo nusu ya idadi hiyo ya watu na maisha yamekuwa magumu hivi, vipi tukifika huko? Msemo wa kuishi kama “Mashetani” naona kama unakwenda kudhihirika.

Wewe unadhani matatizo yapi mengine yatatokea muda huo? Na nini tufanye kama taifa katika kuyakabili?

Ni maoni yangu tu. Siyo lazima uyakubali!
 
Wewe ni miongoni mwa wasomi wengi waliothirika na udanganyifu wa elimu ya magharibi.
Tanzania 1961 ilikuwa na watu milioni 10 sasa 2022 ni angalau million 60 niongezeko la zaidi ya 500%
2050 miaka 28 ijayo makadirio tutakuwa milioni 130 Ongezeko la 100%+
Embu tazama watu kama rasilimali halafu usimezwe sana na propaganda.
Watu ni muhimu sana wakiwa wazalishaji hivyo tazama namna tutaweza kutumia hiyo rasilimali
Binafsi nina mpango wa kuajiri watu milioni 1+ hadi kufikia 2050
 
Ushauri watu tuache kumwaga ndani
Kumwaga nje ni dhambi.
IMG_20220809_123303.jpg
 
Inakuwaje binadamu unakuwa na wasi wasi kwa ongezeko la binadamu mwenzako??

Kama unaona hilo ongezeko linakuoa wasi wasi sitoe uhai mapema sana upunguze hiyo idadi
 
Nakuunga mkono sana huko tuenda ni hatari tupu, kwanza vyakula tulivyo navyo leo havitakwepo na kama vitakuwepo vitakuwa garama sana, mfano kama kuku wa kienyeji kumpata itakuwa shida sana hata mayai yake, matatizo kama magonjwa yataongezeka sana, pia maadili yata shuka sana ushoga ndiyo utashika hatamu. Mwenye maskio na asikie.
 
Wakati Mwingine akili ya ziada inatakiwa hapa ni kweli uchambuzi huu unahekima nzuri sana ya kuvutia lakini jaribu kuwa maisha wanayoishi Bangladesh ambao ukubwa wa eneo la nchi yao ni sawa na Tabora lakin wako watu million 160 na kidogo na maisha yanaenda kama kawaida .Kwanini Tanzania tusiitumie hii kama fursa na sio kama tatizo..Maeneo mengi ya nchi bado yako wazi na yanaihaji watu kuyaishi na kuyafanyia maendeleo.🤔
 
Wewe ni miongoni mwa wasomi wengi waliothirika na udanganyifu wa elimu ya magharibi.
Tanzania 1961 ilikuwa na watu milioni 10 sasa 2022 ni angalau million 60 niongezeko la zaidi ya 500%
2050 miaka 28 ijayo makadirio tutakuwa milioni 130 Ongezeko la 100%+
Embu tazama watu kama rasilimali halafu usimezwe sana na propaganda.
Watu ni muhimu sana wakiwa wazalishaji hivyo tazama namna tutaweza kutumia hiyo rasilimali
Binafsi nina mpango wa kuajiri watu milioni 1+ hadi kufikia 2050

Kikubwa hiyo rasilimali watu ibalance na other resources ,lah sivyo ni hatari.
 
33 Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.
Yohana 16
 
Back
Top Bottom