Tutajuaje kwamba Mkopo wa Daraja la Kigamboni umeisha?

Tutajuaje kwamba Mkopo wa Daraja la Kigamboni umeisha?

Mkataba uliisha mwaka 2022 lakini Kwa kuwa wajanja wamemzidi akili mama yetu,tusitegemee kuacha kutozwa tozo kwenye Hilo daraja
 
Kwani hata mkopo ukiisha ndo mpite bure? maintenance na taa zile bili alipe nani?...

Waendelee kutoza milele...hutaki kulipa pita na baiskeli au na miguu nibure
 
Mkataba uliisha mwaka 2022 lakini Kwa kuwa wajanja wamemzidi akili mama yetu,tusitegemee kuacha kutozwa tozo kwenye Hilo daraja
Hakuna anaetozwa akipita na miguu au baiskeli...wanatoza vyombo vya Moto kulipia maintenance na uchakavu..
 
Pigeni mbizi kwenye bahari mvuke upande mwingine 🐒
 
Infact madaraja makubwa kama busis,,,kigaomboni/Nssf na Tanzanite na mengineyo makubwa ambapo ferry zilikuwa zinatumiwa watu kulipa ni vizrui magari yanayo uka yalipe kama road toll ili kurudisha fedha tuliyojengea ili tujenge madaraja na miundo mingine tena
 
Swali muhimu lingekuwa kufahamu mapato kwa siku na kile kinachodhaniwa ni deni.

Vinginevyo tunachoshana tu hapa.
 
Back
Top Bottom