Udini mbaya sana hasa kwa mtu ambaye unamfagilia halafu hana muda na wewe na yeye ana Imani yake huko na anaamini MUSA ndio Nabii Mkuu na hapaswi kupingwa.
Walipofika nchi ya ahadi,hawakuwa na mtawala mwanadamu,hivyo 'MUNGU' mwenyewe ndio alikuwa mtawala wao na alikuwa anawaletea MWAMUZI ambaye anapokea maagizo kutoka kwa 'MUNGU".
Sasa wazee wa Israel wakamwendea Nabii Samweli wakati huo ndio MWAMUZI,wakamwambia Mataifa mengine yana Wafalme wao mbona sisi hatuna Mtawala,na wewe ndio MWAMUZI lakini watoto wako hawafuati amri na shria za 'MUNGU".
Kitendo hicho kikamuudhi Nabii Samweli lakini 'MUNGU' akamwambia kawaambie watu hao kwa kuwa wamenikataa nisiwe Mtawala wao na wanataka Mtawala mwanadamu, basi Mfalme atawatumikisha, watamwinamia na atawatoza kodi. Hapa ndipo matatizo yalipoanzia hadi kufikia nchi kugawanyika baada ya Mfalme Suleimani kufa.Kukawa na Yuda na Israeli.
Kosa lingine ni baadhi ya Wafalme kuanza kuleta masanamu kwenye HEKALU,na kosa la mwisho ni kumkataa KRISTO,na wakasema damu yake iwe juu ya vichwa vyetu na wana wetu.