Unyayo wa Fasihi
New Member
- Jul 18, 2022
- 1
- 2
Ni nyakati hizi ambazo kila jua likienda zake, Watu Wa Mataifa ya Magaharibi Huumiza kichwa kuona namna gani kesho ikija, wabadili kitu gani kutoka kuwa Ugumu kwenda Kwenye Wepesi, Maana yangu ni kwamba kila uchwao watu wa mataifa yaliyoendelea kiuchumi, kiutawala na kitekinolojia huumiza vichwa vyao kuona namna gani maisha magumu ya jana leo yawe mepesi, na maisha magumu ya leo kesho yawe mepesi, Wenzetu wamewekeza nguvu kwenye Maendeleo Ya Tekinolojia, Kwasababu huko ndiko kuna unafuu na tija ya kukua kiuchumi.
Hapa kwetu kwenye bara la Afrika mambo yamekua tofauti kabisa, Huko Duniani Kuna Tekinolojia Kadha wa kadha ambazo endapo mataifa yetu yangewekeza nguvu kuzikopi hizo teknolojia basi leo tatizo la ajira kwa vijana wetu lisingekua Janga kubwa.
Sipo hapa kueleza kwamba tuwekeze nguvu katika kukopi vya wenzetu na kupuuza vya kwetu. Ukweli ni kwamba kwetu tunao vijana wengi wa bunifu lakini serikali zetu hazijataka kuwathamini hawa vijana kwa kuwapa Nguvu ya mtaji, utaalamu na hata kuziendeleza Bunifu zao.
Afrika kwenye miji mingi na vijiji kuna wabunifu bwelele kama wa Ulaya hata Uchina, ila kwa kua tunakasumba ya kuamini yale ya magharibi ni bora kuliko ya kwetu basi tunajikuta tupo palepale tumesimama wima kila uchwao tukipokea na kukopi Teknolojia za wenzetu kiasi kwamba kuna nyakati tunakopi hata zile ambazo haziendani na mazingira yetu.
Kwangu mimi ni tofauti katika kuamini namna ua njia bora za kuwasaidia vijana wa ki Afrika ambao wametoka Vyuo vikuu na hawana ajira, na pengine hata serikali haijataka kuunda mbinu thabiti za kuwasaidia vijana hao, Basi Mawazo Yangu yatajikita katika Kilimo.
Ndiyo Kilimo kinaweza kikawa ndio sekta namba moja ambayo ikiwekewa nguvu, rasilimali na sera madhubuti basi kwa kiasi kikubwa nchi zetu zitakua zimepunguza janga hili la UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA.
Ni Aibu na Ujinga Leo eti Afrika Inaathiriwa na Vita Vya UKRAINE Na URUSI kwa kukosa NGANO. Yatupasa tujitafakari kwa kina, tuna Ardhi bikra, tuna vijana, tuna mito, tuna kila aina ya rasilimali yakutuwezesha kulima Ngano na kuiiuza nchi zingine. Lakini cha ajabu tumekuwa tukitegemea kila kitu kutoka Magharibi.
Mawazo yangu Katika Kufuta au Kupunguza Tatizo la ajira kwa vijana ni kama ifuatavyo..
1. Kuanzishwe kwa Mashamba ya Kanda Yatakayoitwa "Mashamba Ya Kikanda"( Zone Famrs). Tanzania tuna kanda mbalimbali Kanda ya Nyanda za juu kusini, kanda ya kasikazini, kanda ya magharibi, kanda ya Kati na kanda ya kusini. Hivyo kama serikali Ingeanzisha mashamba ya kanda, kila kanda kukatengwa hekari kadhaa, ambazo zitapewa miundombinu yote ya kilimo, wataalamu, matrekta, mbolea, madawa, nk. Kisha kukfanyika usajili wa vijana au wakachaguliwa vijana kwa kuzingatia idadi, vijana wakakabidhiwa mashamba wakawa wanalima na kuhudumia mashamba, huku serikali ikiwapatia ruzuku na kuwaandalia masoko baada ya Mavuno. Kila kanda ikazingatia zao la kanda hiyo, pakawa na ufatiliaji wa kina, ikawa ni ajenda ya taifa. Na uhakika baada ya miaka mitano serikali inaweza ikawa imepunguza vijana walalamishi na wasio na ajira. Muda mwingine vijana hawana pa kujiairi sababu ya mazingira yanayowekwa.
2. Lazima Serikali, Taasisi, Wadau na Jamii kwa ujumla zitambue kuwa Taifa Imara Ni taifa ambalo watu wake wameshiba, kushiba Kijamii, kielimu, kiafya na kimaarifa. Lakini swala litakaloleta utulivu ni Wanajamii Kuwa Na Uchumi Imara. Lazima Tujikite kuhakikisha pato la mmoja mmoja linakuwa imara. Vijana ili wapate ajira, Serikali inatakiwa kuwekeza nguvu kwenye uchumi wa kidijitali. Elimu ya Uchumi wa kidijitali inabidi ianzishwe mashuleni mpaka chuo kikuu ili vijana wapate ujuzi wa kujitegemea. Leo hii Youtube, Google, Facebook, Instgram ikitumika Vyema kiuchumi vijana wengi watajiajiri. Serikali zetu zimewekeza nguvu kubwa kwenye elimu ya Mkoloni, zama zimebadirika kuna ulazima wa kutafuta mfumo mpya wa elimu ambao utatutoa kwenye Ubutu kwenda kwenye ukali.
Mawazo yangu "ELIMU YA UCHUMI WA KIDIJITALI" serikali iwekeze Nguvu Kubwa Huko.
3. HUB ZA WABUNIFU ZIANZISHWE NA KUWEKEWA NGUVU KITAIFA.
Ni kweli tuna vyuo vya Veta na Tuna SIDO ambako kuna wabunifu mbali mbali. Swala la ukosefu wa ajira limekuwa kubwa kiasi kwamba vijana wengi wamekua walalamishi na serikali haijaweka nguvu kubwa katika kuhakikisha tatizo linaisha. Mawazo yangu serikali ianzishe HuB za kitaifa ambazo zitatumika na vijana wabunifu katika tekinolojia, na serikali kupitia taasisi zake ikawa inatumia HUB hizo kuchagua zile telinolojia mbalimbali ambazo zitakua bora kwa taifa letu, zikaendelezwa na kutumika katika jamii.
4. AFYA.
Pamoja na kwamba duniani kila siku teknolojia zinabadirika na kuvumbuliwa katika nyanja mbalimbali, kuna tatizo kwenye swala la Afya. Serikali nyingi za Afrika zimeshindwa kufanya huduma ya Afya kwa kila raia kupatikana kirahisi. Ukienda vijijini watu wanateseka mno katika kufata huduma za afya, na wanatumia muda mrefu, unaweza kuta mama mjamzito anatembea Kilometa zaidi ya Tisa kuzifata huduma za kliniki. Tunakwama wapi? Kama huduma za kifedha kama M-pesa, Nmb, Crdb, Halopesa zipo ndani ndani huko tunashindwa vipi kufanya huduma za kiafya kuwa karibu na watu?? Nafikiri tumekosa Uthubutu na mawazo mapana.
Mawazo yangu katika afya ili kuwaokoa watu wa vijijini haswa kina mama wajawazito Kuanzishwe "Afya Kiosiki" vibanda au vyovtlyote tutakavyoona inapendeza kila kijiji kukajengwa "Afya Kiosiki" ambacho kitakuwa na huduma muhimu na za haraka kwa wanajamii wanaposumbuliwa na afya. Viosiki hivi vikawekewa miundombinu ya Sola sehemu ambazo umeme haujafika au hata umeme, kisha vijana ambao wapo tu mitaani na degree zao wakawekwa ili kuviendeleza. Serikali ikawa inawapatia ruzuku za uendeshaji. Kwanini hili linawezekana?
Ni hivi
Mimi nimekuwa nikifanya tafiti katika Mkoa wa Tabora, hususani wilaya ya Kaliua, huko Kaliua Kuna Jamii nyingi za wasukuma na wao wanakaa ndani ndani huko ambapo hakuna huduma za kijamii, sasa ili wapate huduma hujikuta wanatembea kilometa nyingi zaidii kuzifata Zahanati, kitu ambacho muda mwingine wamama wajawazito na wagonjwa hupoteza maisha. Kwa serikali zetu za Afrika kujenga Zahanati kila sehemu iliyopo watu imekuwa ngumu. Hivi Viosiki Afya Vitasaidia.
Kuna vijana wengi kadha wa kadha tumewashuhudia kwenye Luninga na YouTube wakionesha bunifu zao za kitekinolojia, lakini serikali haiwapi ushirikiano wa kimtaji na rasilimali ili bunifu hizo zikawe na tija kwa jamii yenye maendeleo thabiti.
Mawazo yangu ni hayo kwa umuhimu wa maendeleo ya Jamii ya Kitanzania na Afrika Kwa ujumla.
#UnyayowaFasihi
0625207262

Upvote
2