Tutarajie nini kipya kutoka kwa bosi mpya wa TTCL?

Tutarajie nini kipya kutoka kwa bosi mpya wa TTCL?

James Hadley Chase

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2020
Posts
1,984
Reaction score
3,695
Juzi usiku ulifanyika uteuzi wa viongozi mbalimbali wa taasisi na tawala zingine. Upande wa shirika la mawasiliano TTCL ameteuliwa bwana MOREMO CHACHA kutoka shirika la uzalishaji mali.
Je, huyu bwana ni nani anaijua historia yake?

Je, atayaweza majukumu ya kuongoza hili shirika mbalo watangulizi wake wamelishindwa kuanzia Waziri Kindamba mpaka Peter Ulanga?

1. Je, atarudisha huduma za kupiga simu, SMS na MB kwa njia za simcard ambazo mtangulizi wake Peter Ulanga aliamua kuua huu utaratibu ili kujikita zaidi kwenye internet za majumbani na ofisini?

2. Meneja Masoko bwana Vedastus Mwita ataendelea kubaki kwenye nafasi yake, maana huyu bwana hana ubunifu kabisa, yupoyupo tu ofisini anapulizwa na kiyoyozi na kusubiria mshahara na posho zingine?

3. Je, ataweza kushugulikia utendajikazi wa baadhi ya wafanyakazi mizigo, mfano unaingia ofisini unakuta baadhi ya wafanyakazi wapo bize kusuka mikeka ya kubeti kwenye kompyuta za ofisi wengine wapo bize kupakua movies na series hasa hawa vijana?

4. Je, atashugulikia uwajibikaji, baadhi ya wafanyakazi hasa hawa huduma ya wateja wana majibu ya shombo sana hawa wanakujibu unavyojisikia. Hata ukiwafuata ofisini kwao ana kwa ana wana majibu ya karaha utadhani wanafanya kazi bure, ukiwa na roho nyepesi unaweza kurusha ngumi bure.

5. Je, ataongeza upatikanaji wa vifaa vya kufunga intaneti majumbani na maofisini?
Kuna watu wamejaza fomu tangu utawala wa JPM mpaka leo hawajafungiwa kila waliripotu mara tunakuja kesho, mara keshokutwa, mara mwezi ujao, mara miezi mitatu ijayo mara mwaka umeisha mara miaka mitatu imeisha.
 
Kama ni fiber wanafunga kwa awamukatika maeneo wanaona ni potential. Kama upo nje ya hayo maeneo ni kalenda tu kwenda mbele.
 
Back
Top Bottom