Adverse Effect
JF-Expert Member
- Oct 8, 2017
- 2,049
- 5,449
Wale wote wenye nia njema na wanaochukia uonevu na unyanyasaji wanaofanyiwa wenzetu jamii ya wamasai tuwaunge mkono kwa kuvaa mavazi yao ya asili.
Uhamasishaji mkubwa utafanyika kuhakikisha nguo na mavazi kama lubega au mashuka ya wamasai yanavaliwa na wote ambao tunawapenda na kuwajali wenzetu.
Zoezi hili litakuwa endelevu sababu limepata baraka na kibali kutoka kwa mamlaka iliyopo juu ya mamlaka zote.
Ukombozi umekaribia, sakata la wamasai na ngorongoro linakwenda kutufanya tuungane na tuwe kitu kimoja na nia moja.
Wakati ukifika hata wenzetu wa ulinzi na usalama watajikuta wamevaa nguo na mavazi ya wenzetu wamasai sababu watakuwa wameujua ukweli na ukweli utawaweka huru.
Serikali ya Rais Samia ikumbuke na isisahau kuwa wamasai ni rafiki wa kila jamii na kila taifa lolote duniani.
Kama wamasai wanaweza kuishi na tembo, Simba, chui na wanyama wengine basi tutambue kuwa wamasai wana upendo na utulivu mkubwa sana waheshimiwe.
Hakika wamasai watashinda.