1.
Shime shime wananchi, mabingwa kihistoria,
Jambo letu la kinchi, hakika limewadia,
Ni ile yetu mechi, nyepesi kupindukia,
Tawapiga kama ngoma, Makolo nawaambia.
2.
Tukaujaze uwanja, yapatikane mapato,
Tujivutie mkwanja, tukiongeze kipato,
Tukiacha janjajanja, hautotokea msoto,
Tawapiga kama ngoma, Makolo nawaambia.
3.
Yanga ikisonga mbele, Makolo yanaumia,
Kwetu daima mbele, nyuma hatutasalia,
Kwanza tuna Mayele, sioni wakumzuia,
Tawapiga kama ngoma, Makolo nawaambia.
4.
Na mtaisoma namba, hiyo siku kwa Mkapa,
Tena haina mbambamba, Makolo tutawachapa,
Si iliwashika hamu, zamu yenu ishafika,
Tawapiga kama ngoma, Makolo nawaambia.
5.
Na tena mlete timu, siku itakapofika,
Mjibebee na ndimu, mana mtatapika,
Si iliwashika hamu, zamu yenu ishafika,
Tawapiga kama ngoma, Makolo nawaambia.
6.
Twasubiri kutetema, tarehe ishina tatu,
Bila hata ya huruma, Tutawanyukeni tatu,
Kulia Shabani Djuma, Mutambala namba tatu,
Tawapiga kama ngoma, Makolo nawaambia.
7.
Litakuwepo langoni, Nyanda dakaji mishale,
Litombo naye Kapiteni, Azizi pia Mayele,
Wanangu wa Jangwani, embu pigeni kelele,
Tawapiga kama ngoma, Makolo nawaambia.
8.
Katikati babu kaju, yani kiungo bamia,
Nalo zee la mikwaju, Zawadi mwana Mauya,
Si ndumba wala juju, hamna pa kutokea,
Tawapiga kama ngoma, Makolo nawaambia.
9.
Nje ya kumi na nane, mtoto Fei mwamjua,
Mishuti mwana ukome, hupenda kujipigia,
Na migoli ya karne, hachoki kutupia,
Tawapiga kama ngoma, Makolo nawaambia.
10.
Mipasi ya mchomoko, kwa wingi tutazipiga,
Zitagongwa mokomoko, na majalo kuyamwaga,
Atamimina Moloko, vichwa navyo kuvipiga,
Tawapiga kama ngoma, Makolo nawaambia.
11.
Ni mtumbwi wa vibwengo, Makolo mlovamia,
Wenu Kocha wa mchongo, tamati yakaribia,
Kwa niijuavyo Bongo, mkeka keshachaniwa,
Tawapiga kama ngoma, Makolo nawaambia.
12.
Tena bado liko moto, letu jopo la ufundi,
Waandaa mkong'oto, Nabi na yule Mrundi,
Mjue siyo ndoto, tunaingia makundi,