ANDINIKA USHINDE
Nina wazo na nikaona ni vyema niliwakilishe kwenu, hata kama sio mahali sahihi mtanisaidia lifike penyewe. Nimekuwa nikiona majanga mengi yatokanayo na mvua kama mafuriko na hakuna jitihada zinazotumika kukabiliana na hali hiyo.
ANDIKO
MABWAWA KUZUIA MAFURIKO
Kila mara huwa tunashuhudia kwenye msimu wa mvua tunapitia changamoto nyingi za mafuriko na kusababisha maafa makubwa ya vifo na uharibifu wa miundo mbinu, nyumba na mashamba. Baada ya msimu wa mvua kupita tunaanza kupata kiangazi na hivyo kukosa maji majumbani, mashambani na kwenye mabwawa ya kufua umeme.
Hilo jambo linakera sana na linasababishwa na kutokuwa na miundo mbinu ya kuhifadhi ziada ya maji ambayo hutuletea shida na baadae hupotea bila faida yoyote. Nashauri sasa kuwa ni vyema sasa tuje na ujenzi wa mabwawa makubwa ya kuweza kuhifadhi hayo maji yanayosababisha mafuriko.
Mabwawa hayo yajengwe maeneo yanayokumbwa zaidi na mafuriko na hata sehemu zisizo na mafuriko lakini kuna mito inayopeleka maji baharini na yawe kwenye muinuko ili iwe rahisi maji kutiririka yanapofunguliwa kwenda mashambani kwa matumizi ya umwagiliaji kwenye msimu wa kiangazi na kuweza kuzalisha mazao ya chakula mwaka mzima au popote maji yatakapohitajika kama viwandani.
Mabwawa yawe na mlango wa kuingilia maji na mlango wa kutolea inayoweza kufunguliwa na kufunga. Matumizi ya maji haya ni kwa umwagiliaji, umeme, mifugo, kufuga samaki, maji ya kunywa, viwandani na usafiri. Mabwawa yanawekwa milango ya kufungulia maji kwenda mashambani kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji, kwenda kuongeza nguvu kwenye bwawa la kufua umeme kama kiwango cha maji kimepungua au kwenda kwenye mitambo ya kuchujia maji ya matumizi majumbani.
Pia haya mabwawa yataingiza pesa kutokama na usafiri au ufugaji wa samaki na kilimo cha kibiashara. Mabwawa haya yatakuwa chini ya uangalizi wa Serikali au serikali itapanga utunzaji kama itakavyoona na patajengwa sehemu ya kusafishia maji, mashine ya kutengeneza vyakula vya samaki watakaofugwa humo na ofisi ya msimamizi na mlinzi.
Msimamizi atahusika na uangalizi wa matumizi ya mabwawa, makusanyo ya mapato toka kwa wavuvi, usafiri na mauzo ya maji ya majumbani. Haya mabwawa yatakuwa miradi mikubwa sana ya kiuchumi kwa serikali na hivyo kuchangia pato kiuchumi. Haya ndio mawazo yangu.