SoC04 Tutengeneze mazingira rafiki kwa wawekezaji kupunguza ukosefu wa ajira

SoC04 Tutengeneze mazingira rafiki kwa wawekezaji kupunguza ukosefu wa ajira

Tanzania Tuitakayo competition threads

BabaMorgan

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
4,869
Reaction score
13,137
Ukosefu wa ajira ni miongoni mwa changamoto sugu ulimwenguni kama taifa yatupaswa kuwa na mikakati mipya na endelevu kupunguza ukosefu wa ajira nchini.

images (3).jpeg

Bendera ya Tanzania.

Kila mwaka mamia ya wahitimu wanatunukiwa vyeti vya kuhitimu katika kozi mbalimbali kutoka vyuo vya ndani na nje ya nchi ukweli mchungu ni kuwa serikali haina uwezo wa kuajiri Kila mhitimu kutokana na ufinyu wa nafasi katika taasisi za serikali kulinganisha na idadi kubwa ya wahitimu kutoka vyuo mbalimbali.

8.jpg

Wahitimu Tanzania

Serikali kupitia wawekezaji na wadau kwa kushirikiana wanaweza kupunguza ukosefu wa ajira nchini. sekta binafsi ikipewa nguvu na kutengenezewa mazingira wezeshi basi wahitimu wengi watapata ajira zitazowawezesha kupata kipato cha kukidhi gharama zao za maisha.

Uwepo wa wawekezaji wengi wakubwa katika sekta tofauti kama kilimo na viwanda nchini kutasaidia kwa kiwango kikubwa kumaliza tatizo la ukosefu wa ajira.
images (6).jpeg

Kiwanda Cha sukari.

Je ni nini kifanyike na serikali yetu kuweza kuvutia wawekezaji wakubwa kuja kuwekeza Tanzania?

1. Kutangaza fursa zinazopatikana Tanzania. Katika vitu Tanzania tunapaswa kujivunia nacho basi ni bandari imerahisisha kufanya biashara za kimataifa. Kwa faida hiyo ni jukumu la Kila Mtanzania popote pale alipo kutangaza fursa zinazopatikana Tanzania kama vile kilimo, madini na utalii pia mabalozi wetu watumie uwepo wao katika mataifa wanayotuwakilisha kutangaza Tanzania lengo kuu ni kuvutia wawekezaji wakubwa kuja kuwekeza Tanzania.
images (7).jpeg

Bandari Dar es salaam.

2. Kupunguza mlolongo na uchelewashaji usio na tija kwenye usajiri na uanzishwaji wa kampuni.
Pamekuwa na malalamiko mengi juu ya taasisi zilizopewa mamlaka ya kutoa vibali vya uwekezaji kwa makusudi kuchelewesha na kutengeneza mianya ya rushwa kwa wawekezaji wapya kimsingi katika ulimwengu wa Sasa muda ni rasilimali muhimu panapokuwa na mlolongo mrefu katika usajiri wa kampuni tunapunguza morali ya wawekezaji kuja huku wengine wakikata tamaa na kuishia njiani. Pawepo na uadilifu kwa maafisa wetu wote kwenye mamlaka zetu.

3. Msamaha wa Kodi katika mitambo ya uzalishaji inayoingia nchini. Kimsingi uwekezaji ni gharama kubwa kama serikali inabidi kuwashika mikono wawekezaji kwa kuwapunguzia gharama hususani Kodi mamlaka ya mapato Tanzania itoe misamaha ya Kodi kwa mitambo ya uzalishaji inayoingia nchini ili kuchochea uanzishwaji wa viwanda vingi.

4. Uongozaji wa haki na demokrasia. Wawekezaji kabla ya uwekezaji ufanya tathmini juu ya uongozi wa sehemu husika kujua ni aina gani ya uongozi unafuatwa tukiwa na uongozi wa haki utachochea wawekezaji kuja kwa wingi
images (5).jpeg

Bendera za vyama vya siasa Tanzania.

5. Uboreshaji wa miundombinu ya usafiri, maji, umeme na huduma za kijamii kama vile elimu na afya.
Muwekezaji anashawishika kuwekeza mahali ambapo Kuna uhakika wa upatikanaji wa huduma muhimu kama maji, umeme na miundombinu ya barabara zinazopitika wakati wowote
images (4).jpeg

Morogoro Road.

Hakika tukifanya haya basi tutawavutia wawekezaji wengi kuja nchini mwetu kuwekeza na kupunguza ukosefu wa ajira nchini.

Picha zote chanzo Mtandaoni
 
Upvote 2
umeleta mawazo chanya na muhimu sana, tumeona mfano wa bagamoyo suger, tumeona wafanyabiashara wakubwa wakipewa mazingira mazuri ya uwekezaji wanaweza kuinua uchumi wa nchi na kutengeneza ajira.

serikali ingetenga bil 500 kila mwaka kuwawezesha wawekezaji wakubwa. ipo miradi mikubwa inayo hitaji kupelekewa maji umeme na barabara tu vingine mwekezaji atamalizia mwenyewe,
 
Shida ni kwamba sisi tunafanya kazi kwa kujilinganisha. Yan kwa Tz sio ajabu kumwona kiongozi akisema mbna hata kenya kuna tatizo la ajira. Ajira zipo ila shida ni uswahili na busines as usual yan huwez amini hata ajira za muda wanatumika watumishi wa serikali, kwenye zoezi la sensa walijitahid kdg japo watumishi walipata pia, sas akama sasa hvi KUBORESHA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA wamechukuliwa hadi walimu na ma clinical officer?? kweli hapo tupo serious au tunatania mwlm ana mshahara anaacha kaz ya kufundisha kwa ajili ya kazi ya laki tatu na nusu, kwa nini hii kazi asipewe kijana ambae n jobless ambae akipata hii 350k anaweza kupata hata mtaji wa kuanzisha biashara ya kuuza karanga?? mwl, anaacha kufundisha wiki nzma kisa daftari la mpiga kura kweli?? tubadilike na iwe sheria
 
Back
Top Bottom